Na Mwandishi Wetu,TimesMajira Dar es Salaam
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (PCCB) Mkoa wa Ilala, Dar es Salaam imeokoa na kudhibiti fedha kiasi cha shilingi Billioni 1,037,207,090 zikiwa ni fedha za Mfuko wa Taifa wa Pembejeo ( AGITF) na Mfuko wa Huduma wa Hifadhi ya Jamii (PSSSF).
Hayo yamesemwa mkoani Dar es Salaam jana na Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Ilala, Christopher Myava wakati alipokuwa akitoa taarifa ya utendaji kazi kwa umma katika kipindi cha kila robo mwaka Januari hadi Machi.
Amesema, mfuko wa Taifa wa Pembejeo ulitoa fedha kwenye benki mbalimbali ili wazikopeshe kwa wakulima, lakini fedha hizo hazikurudishwa katika mfuko huo hata baada ya wakulima kuzirudisha fedha hizo kwenye benki walizokopa.
Myava amesema, kitendo hicho kinatafsiriwa kama cha kujinufaisha kwa kutumia fedha za Serikali kinyume na sheria ya Kuzuia na Kupambana Rushwa Na. 11 ya mwaka 2007, ambapo mpaka sasa fedha zilizorejeshwa kwa miezi mitatu ni shilingi millioni 688,278,090.
“Mfuko wa Huduma wa Hifadhi ya Jamii (PSSSF) walizikopesha SACCOS za taasisi mbalimbali ili wakopeshe kwa wanachama wao baadae wazirejeshe PSSSF, lakini hazikurejeshwa ambapo kiasi kilichorejeshwa kwa kipindi cha miezi mitatu ni shilingi millioni 348,909,000 na fedha ambazo hazijarushwa tutaendelea kuzifuatilia ili zirejeshwe serikalini,”amesema Myava.
Vilevile amesema katika kipindi cha Januari hadi Machi 2021 TAKUKURU Mkoa wa Ilala imefungua kesi mpya nne na mashauri 22 yanaendelea mahakamani.
Myava amesema, mashauri hayo yalioko mahakamani ni pamoja na shauri la Mamlaka ya Mapato (TRA) manne, Serikali za mitaa mashauri manne, wafanyabishara matatu, Idara ya Afya matatu,ujenzi mawili, elimu ya juu moja, ardhi moja, vyama vya siasa mawili, maji moja na aliyekuwa mtumishi wa TAKUKURU moja.
More Stories
Serikali kupeleka mawasiliano maeneo ya mipakaniÂ
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best