Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline,Gairo
MKUU wa Taasisi Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU)Wilayani Gairo imesema inalengo la kupeleka kliniki tembezi ya kutia elimu ya kuzuia na kupambana na rushwa wilayani gairo Mkoani Morogoro inatarajiwa kuwafikia wananchi wa kata 18 zilizopo wilayani humo kabla ya kwenda kwenye zoezi la kampeni za vyama vya Siasa katika kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao mwaka huu.
Kauli hiyo imetole leo Februari 26,2025 na Mkuu wa taasisi hiyo wilaya ya Gairo Julieth Mtuy wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii ambapo amesema wao kama Ofisi ya TAKUKURU wilaya wameshajipanga kutoa Elimu ya kuzuia na kupambana na rushwa wilayani gairo wakati wa kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao.
“Sisi kama taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa tumekusudia kufikisha Elimu kwa wananchi wote wa wilaya ya Gairo kwa kutumia kliniki tembezi kwa kila kata lengo kubwa ni kuwaelimisha wananchi jinsi ya kuzuia na kupambana na rushwa katika kipindi chote cha kampeni za vyama vya Siasa katika kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao hapa nchini kwakuwa tukiwafikia huko walipo kwenye kata zao na vijiji na vitongoji vyao ili waepukane na dhana ya kupata kiongozi bora hadi wapewe rushwa hili jambo halikubaliki kabisa”amesisiza Mtuy
Mtuy amesema kuwa kuelekea kampeni za vyama vya Siasa huwa kunajitokeza watu wachache wasio waadilifu na wazalendo wa Nchi wanakuwa wakitafuta vyeo kwa kutoa rushwa jambo ambalo ni kinyume cha sheria na katiba ya nchi yetu.
“Ukifika muda wa kampeni za vyama vya Siasa utaona baadhi ya watu wanaowania nafasi mbalimbali wanazitafuta nafasi hizo kwa kushawishi wananchi wawachague kwa sababu wanatoa rushwa Sasa kwa hapa Gairo wajipange kwa kushirikiana na vyombo vingine tumejipanga kuhakikisha suala la rushwa hatulipi nafasi hapa wilayani gairo hata kidogo”amesema Mtuy.
Amesema kliniki tembezi ambayo itatembea kata zote 18 kwa lengo la kutoa Elimu kwa wananchi Juu ya viashiria vya rushwa vikoje inalenga kuwajengea uwezo wananchi na viongozi kwenye kata zote ili kila moja apate uelewa na kuona rushwa ni adui mkubwa lazima tupige vita suala hilo.
“Hii kliniki tembezi naimani itatuletea mafanikio makubwa kabla ya kuelekea kwenye uchaguzi Mkuu nasi kama taasisi tumejipanga vizuri kuhakikisha Elimu hii ya kuzuia na kupambana na rushwa inafika kila kona na makundi mbalimbali wilayani hapa na tumeshaanza na kundi la Viongozi wa Dini na tutaendelea na makundi mbalimbali wilayani hapa yakiwemo wanasiasa,walemavu,wanawake, Mama lishe na Baba lishe,vijana na watu wenye ulemavu lengo ni kila moja ajue umuhimu wa kupinga rushwa katika maeneo yake”
Mtuy amesema suala la rushwa ni suala mtambuka hivyo wao kama TAKUKURU watahakikisha macho na masikio wameyatega vizuri ili kuhakikisha wanawabaini wote watakao husika kutoa na kupokea rushwa kwani wote ni wakosaji.
More Stories
Said :Miundombinu ya maji mkunduge mambo safi
Wadau wakutana kwa tathimini maendeleo ya Elimu
JKCI:Tiba Mkoba ya Dkt.Samia yawafikia watu 21,324