Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online DSM
TIMU ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” imefufua matumaini ya kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2023 yatakayofanyika nchini Ivory Coast baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Niger
Mshambuliaji wa Taifa Stars Saimon Msuva mfungaji wa goli pekee ndiye shujaa wa mchezo huo wa kutafuta kukata tiketi ya kufuzu fainali za afcon uliyochezwa juni 18, 2023 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma amewaongoza watanzania kuishangilia timu yao akiwa Mgeni Rasmi katika mchezo huo hatua iliyoongeza hamasa.
Mchezo huo umeshuhudiwa pia na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Saidi Yakubu na Naibu Katibu Mkuu wake Nicholas Mkapa, Rais wa Shirikisho la Mpira nchini (TFF) Wales Karia.
Tanzania ipo kundi F ikishika nafasi ya pili na alama 7 na Algeria wakiongoza kundi hilo wakiwa na alama 15, huku Uganda nafasi ya tatu wakiwa na alama 4 wakati Niger wakishika mkiya kwenye kundi hilo wakiwa na alama 2.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi