January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tafiti zaonyesha Chembe chembe za plastiki zenye kemikali hatarishi

Na David John, TimesMajira Online

MATOKEO ya Utafiti uliofanywa na mashirika ya Kimataifa ya IPEN na Pellet Watch kwa kushirikiana na Shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na utunzaji wa Bioanuai Tanzania ( TABIO) pamoja na Agenda umebaini nchi nyingi katika Bara la Afrika plastiki zinazotengenezwa kwa matumizi mbalimbali kuna kiasi kikubwa cha kemikali hatarishi kwa afya za binadamu na Mazingira.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu Utafiti huo Abdallah Ramadhani ambaye ni Mratibu wa TABIO amefafanua matokeo ya utafiti ambayo sampuli zake zilikusanywa katika fukwe za Dar es Salaam kwa lengo la kuangalia chembechembe zinazotumika kutengeneza plastiki kama zina sumu kiasi gani.

“Hizo chembe chembe za plastiki zilikusanywa katika fukwe za Dar es Salaam na kupelekwa nje ya nchi kwa uchunguzi wa kimaabara, sasa matokeo yameonesha kwa Tanzania hizo chembe chembe (pellets) ambazo zilipatikana japo sio kwa kiasi kikubwa, matokeo yalionesha sisi uchafuzi unatokana na chembe chembe hizo katika fukwe ni wa kiwango cha chini mpaka cha kati.

“kemikali zilizofanyiwa utafiti n pamoja na.Brominated flame retardants (used in electronics, bisphenol A eg.used in polycarbonate plastic. Uv-stabilizers (used to prevent deterioration from sunlight ambapo pia baadhi zilipigwa marufuku na mikataba ya Kimataifa katika matumizi.

Amesema kuwa uwepo wa hizo kemikali chafu katika plastiki ambapo zinapokwenda kutengenezwa viwandani /kurejeleshwa (recycling) kama haziondolewi zitaendelea kuwapo katika bidhaa mbalimbali za plastiki na mnajua kwa Tanzania bado matumizi ya plastiki kwa ujumla wake yanaendelea ukiondoa zile ambazo zilipigwa marufuku na Serikali kwa sababu ya kutokidhi viwango na ubora vya utoaji huduma, amesema Abdallah.

Ameongeza kuwa matumizi ya plastiki bado ni makubwa yakiwemo ya vifungashio kama vya maji ,mifuko mbalimbali inayotumika kufungashia bidhaa na iwapo kama bidhaa zinazotoka na plastiki hazijafanyiwa uchunguzi na mamlaka husika kama TBS ,NEMC na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali kujua kwamba hizo plastiki zina kemikali rafiki wa mazingira na kwa afya za Watanzania kwa kiasi gani, basi zitakuwa katika hali hatarishi.

“Kwa hiyo matokeo ya utafiti kama nilivyozungumza hapo awali kemikali hatarishi zipo kwenye plastiki na kwa bahati mbaya hasa katika nchi za Afrika uwezo wa kuziondoa ni mdogo au haupo ,kwa hiyo cha muhimu kinachotakiwa kwamba Serikali isimamie bidhaa zinazotokana na plastiki zikiwa mpya au zile ambazo zimerudishwa kutengenezwa tena viwandani zioneshe kwamba hizo kemikali hatarishi ambazo zimeorodheshwa basi zisiwepo, ziwe zinaondolewa katika bidhaa za plastiki ili kuondoa athari za kimazingira na kwa afya ya walaji.

“Kama plastiki hazina chembe chembe zenye kemikali hatarishi hazina shida, lakini kwasababu hizo chembe chembe zimetolewa zinaonekana zina hizo kemikali sumu hasa zile zinazoongezwa wakati wa kutengeneza plastiki ndizo zinazoleta changamoto. Kama nilivyosema huu utafiti umefanyika kwenye nchi 35 duniani na Tanzania ikiwemo

“Kutokana na muhutsari wa hii ripoti inaonesha nchi za Afrika zimeathiriwa zaidi pamoja na kwamba hazizalishi plastiki kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na nchi zilizoendelea , kwasababu nchi zilizoendelea zina mazingira mazuri ya kusimamia sheria zao, zina teknolojia ya hali ya juu kuondoa hizo kemikali za sumu kwenye plastiki zinazozalishwa tofauti na sisi huku,”amesisitiza.

Pia amesema kuwa kwa Tanzania kwenye matokeo hayo haikuwa juu sana ingawa kuna kiwango cha chini hadi cha kati cha uwepo wa kemikali hatarishi , kwa hiyo Serikali iangalie na kutambua hizo kemikali ambazo ni hatarishi ambazo zinaongezwa (additives) katika kutengeneza plastiki na ikiwezekana kuwe na mbadala na hizo kemikali hatarishi ziondolewe na kupigiwa marufuku katika matumizi hayo.