January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TAFINA: kuvutia wawekezaji nchini

Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online DSM

KATIKA kuunga mkono juhudi za Serikali kwenye sekta ya uwekezaji nchini, Mtandao wa umoja wa wanachama watoa huduma za kifedha kwa njia ya Teknolojia (TANZANIA FINTECH ASSOCIATION – TAFINA) wamejipanga kuhakikisha wanawaongezea mitaji wadau wa maendeleo na kuweka mazingira rafiki ya kisera ili kuvutia wawekezaji katika kuboresha maisha ya Watanzania na kuwainua kiuchumi.

Ameyasema hayo Jijini Dar Es Salaam wakati uzinduzi wa Tanzania Fintech Association (TAFINA) Katibu mkuu wa Tafina Shadrack Kamenya, kuwa dhima kubwa ya uanzishaji wa Tafina ni kuhakikisha kuna kuwepo na umoja wa watoa huduma na kuvutia wawekezaji katika kuboresha maisha ya Watanzania na kuwainua kiuchumi.

Aidha, Katibu mkuu wa Tafina Shadrack Kamenya amesema kuwa umoja huo tayari una wanachama zaidi ya 50 na wamejipanga kutoa fursa kwa makampuni mengine kujiunga katika kuhakikisha watoa huduma bora na rafiki kwa Watanzania pamoja na kufuata misingi yote ya kisheria.

Kwa upande wao baadhi ya wanachama wakizungumza na Timesmajira TV Aisha Said na Evans Makundi – Mkurugenzi Mkuu wa Evmark Tanzania wamesema umoja huo utawasaidia kuweza kushirikiana katika kubadilisha mawazo ya kibiashara na kuendelea kuwa pamoja katika uwekezaji nchini.