December 30, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mkuu wa kitengo cha mawasiliano TAEC Peter Ngamilo akizungumza na waandishi wa habari kwenye mashindano ya MAKISATU

TAEC yatarajia kuanzisha mradi mpya wa teknolojia ya kuhifadhi mazao

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

TUME ya Nguvu ya Atomiki nchini (TAEC)inatarajia kuanzisha mradi wa kutumia teknolojia ya nyuklia katika kuhifadhi vyakula cha  mazao ili kuongeza muda,matumizi na kukikinga dhidi ya uharibifu unoweza kusababishwa na vimelea vya vijdudu.

Teknolojia hiyo itatumika kuboresha bidhaa za viwandani na bidhaa za matibabu (Medical Sterilization).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kwenye mashindano ya Sayansi ,Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) 2021 Peter Ngamilo amesema pamoja na mambo mengine TAEC imeshiriki mashindano hayo kuonyesha kazi zao kwa wananchi lakini pia kuwaonyesha namna wanavyoweza  kutumia teknolojia hiyo mpya ya kuhifadhi mazao ya kilimo bila kuharibika kwa haraka.

 “Takriban nchi 62 duniani zinatumia teknlojia hii mpya ya Nyuklia kuhifadhi mazao mbalimbali ya vyakula vikiwemo vitunguu ,nyanya,maziwa na mazao mengine mengi na kwamba teknolojia hii inahifadhi mazao muda mrefu tofauti na teknolojia nyingine zinazotumika katika kuhifadhi vyakula.”amesema Ngamilo

Naye Mtafiti Mwandamizi wa TAEC Simon Mdoe amesema kwa mujibu wa tafiti asilimia 40 ya mazao uharibika kabla haijamfikia mlaji .

Aidha amesema kutokana na teknolojia hiyo itamwezesha mkulima na wananchi kwa ujumla hata kuingia katika ushindani wa soko la nje yanchi  kwani watakuwa na uhakika wa mazao yao.

Mdoe amesema,mradi wa kutengeneza mtambo huo unatarajiwa kukamilika baada ya miaka mitatu kuanzia sasa.