Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
MKURUGENZI Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomic (TAEC) Profesa Lazaro Busagala amesema,kuanzia mwaka huu Mamlaka hiyo itapeleka vijana watano nje ya nchi kwa ajili ya kusomea masuala ya sayansi ya nyuklia.
Akizungumza jijini Dodoma katika Siku ya TAEC iliyoambatana na maonyesho ya wiki ya Ubunifu ,Mkurugenzi huyo amesema,lengo ni kuendelea kuongeza wataalam zaidi wa sayansi ya nyuklia.
Aidha alisema kumekuwa na changamoto ya wataalam wanawake wenye ujuzi wa masuala ya sayansi ya nyuklia ambapo kufuatia changamoto hiyo TAEC imefanya jitihada za kuwakusanya wanawake ili iweze kuwahamasisha hasa walio shule za sekondari ili baadaye kupata watumishi wenye ujuzi mkubwa wa sayansi ya nyuklia.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi ,Teknolojia na Ubunifu Profesa Maulilio Kipanyula , ameitaka TAEC kuwekeza zaidi katika utafiti ili kupata bunifu nyingi hasa kwenye eneo la Sayansi ya Nyuklia kwani ni muhimu sana katika ulimwengu wa sasa wa teknolojia kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi.
“TAEC mna kazi kubwa sana ya kuhakikisha mnafanya tafiti zaidi kwenye eneo la sayansi ya Nyuklia kwani karibia ulimwengu wote sasa umegekia huko na lengo ni kukuza uchumi wa nchi na naamini kupitia maonesho haya wananchi watapata nafasi ya kuijua zaidi tume hii,”amesema
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Tume hiyo,Profesa Joseph Msambichaka ameitaka tume ya Atomiki kufanya bunifu nyingi zinazotokana na nyuklia kwani Tume hiyo ina uhitaji wa vifaa vingi vyakutosha.
More Stories
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili
ACT-Wazalendo,waitaka Polisi kutobeba chama kimoja