Na Esther Macha, Timesmajira, Online, Mbeya
TAASISI ya Utafiti wa zao la Kahawa nchini (TaCRI) imesema kuwa imedhamiria kuwafikia wakulima 8000 hadi 10000 wa zao la kahawa kutoka maeneo mbalimbali nchini ambao watafundishwa namna ya kuhudumia kahawa ili kuleta tija na uzalishaji utakaochangia ukuaji wa pato kwa mkulima.
Hayo yamesemwa leo na Meneja Program za Utafiti TaCRI Kanda ya Mbeya, Dkt.Dismas Pangalasi wakati Akielezea mikakati waliyojiwekea katika kuhakikisha teknolojia na elimu kuhusiana na zao hilo zinawafikia wakulima.
Dkt. Pangalasi amesema wana udongo nchi nzima kwa kuandaa makala na taarifa mbalimbali zinazoelezea mahitaji ya virutubisho katika kila kipande cha ardhi,” alisema Dkt. Pangalasi.
Aidha Dkt Pangalasi amesema mahitaji ya miche ya kahawa ni makubwa kuliko uzalishaji wenyewe kutokana na ukata wa fedha, hali inayosababisha wakulima kushindwa kulima mazao ya kutosha.
“TaCRI tunajivunia mafanikio ya utafiti wetu ambapo kwa kipindi cha miaka 19 tumefanikiwa kugundua aina 19 bora za kahawa arabika na aina tano za rubusta ambazo zimekuwa zikifanya vizuri sana kwa wakulima wetu, vilevile tumefanikiwa kufanya upembuzi”amesema.
“Nane nane ya mwaka huu tumekuja na mtaala wa kufundishia zao la kahawa ambapo wataalam wetu watakuwa wanawafundisha wakulima miongozo mbalimbali ya namna wanapaswa kufuatilia ili kupata tija kwenye zao la kahawa,” amesema Dkt. Pangalasi.
Ameongeza kuwa wamejipanga kuonesha aina 19 za mbegu bora aina ya rabika ambazo zimebuniwa nchini na taasisi hiyo na kwamba zina sifa mbalimbali kama vile kuwa na vionjo tofauti kulingana na mahitaji ya soko la dunia pamoja na virutubisho .
Sambamba na hilo pia amesema waleta mbegu nyingine mpya tatu aina ya chotara ambazo zinafanya vizuri sana kwa kuzalishaji mavuno mengine na kuhimili hali ya hewa ya ukanda wa nyanda za juu kusini.
Amesema mbegu hizo ni miongoni mwa mbegu zilizobuniwa katika kipindi cha miaka 19 ya utafiti uliofanywa na TaCRI na kusaidia hadi sasa kupata aina 24 za mbegu zilizobuniwa.
Hata hivyo Dkt. Pangalasi amesema wamedhamiria kuwafikia wakulima 8000 hadi 10000 wa zao la kahawa kutoka maeneo mbalimbali nchini ambao watafundishwa namna ya kuzihudumia kahawa ili kuleta tija na uzalishaji utaochangia ukuaji wa pato kwa mkulima.
Kutokana na hali hiyo aliiomba serikali na wadau wengine kuendelea kuwapatia fedha kwa ajili ya kuzalisha miche mingi itayaokidhi mahitaji ya wakulima na kuongeza uzalishaji.
Daines Juma ni mkulima wa zao la katika wilaya ya Mbeya Mbozi anasema uwepo wa Taasisi hiyo umekuwa msaada kwa wakulima katika kuwapatia miche bora ya kahawa.
More Stories
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano
Waziri Chana amuapisha Kamishna uhifadhi NCAA, ampa maagizo mazito
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari