Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais ,Menejimenti ya Utumishi wa Umma wa Umma na Utawala Bora George Simbachawene ameziagiza taasisi za umaa kununua mifumo ya Tehama inayotengenezwa na Serikali Mtandao (e-GA) badala ya kuendelea kununua mifumo ya nje ya nchi.
Simbachawene ameyasema hayo jijini Dodoma alipofanya ziara ya kutembelea kituo cha Utafiti, Ubunifu na uendelezaji Mifumo cha Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) kilichopo Chuo Kikuu Cha Dodoma Ndaki ya CIVE.
” Taasisi yetu ya e-GA inabuni na kujenga mifumo mbalimbali ambayo ofisi za Serikali inaweza kuinunua na kuitumia katika kurahisisha utendaji,naomba nitoe rai,taasisi zije kununua mifumo ya e-GA.”amesema Simbachawene na kuongeza kuwa
“Matumizi ya TEHAMA ndiyo muhimili wa mapinduzi ya Nne ya Viwanda, pamoja na matumizi ya TEHAMA, Ubunifu ni moja ya nyanja Muhimu Sana katika kuendeleza na kuharakisha ukuaji wa uchumi wa kidijitali nchini Tanzania.”
Akitolea mfano wa moja ya mifumo iliyojengwa na e-GA wa e-Mrejesho Simbacahwene amesema,mfumo huo humrahisishia mwananchi kutoa kero zake ,maoni mbalimbali lakini pia hata kuipongeza serikali pale inapofanya vizuri badala ya kutoka sehemu alipo na kwenda ofisi husika .
“Kwa hiyo wananchi wanapaswa waeleshwe kuhusu hii mifumo,naona hapa mnao hata mfumo wa social media wa Oxygen ambao unachat kama watu wanavyochat Whatsapp na mitandao mingine,mifumo yote hii inapaswa kueleweka vyama na wananchi ili waweze kuitumia .”
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa e-GA Mhandisi Benedict Ndomba amesema Kituo hicho kinafanya tafiti kwenye maeneo yote ya TEHAMA hasa kwenye Teknolojia zinazochipukia kama vile Bloc Chain, Artificial intelligence, Machine Learning, Cyber Security na Digital Currency.
Mkurugenzi huyo amesema kupitia Ubunifu, Utafiti na mazoezi kwenye maeneo hayo huifanya nchi kuwa katika nafasi nzuri ya kushindana kwenye uchumi wa kidijitali.
More Stories
Muhoji Sekondari kumaliza changamoto ya umbali kwa wanafunzi Musoma vijijini
Tanzania mwenyeji mkutano wa nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika
TANESCO yarudisha shukrani kwa jamii