Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala
TAASISI ya kijamii TUWODO imepata mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake katika kusaidia Wanawake, Vijana na Watu Wenye Mahitaji maalum katika masuala mbali mbali yanayowazunguka katika maeneo yao hasa kwenye kuendesha mafunzo kwa majukwaa ya wanawake juu ya sheria ya mtoto na mafunzo ya binadamu na Utawala bora.
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Taasisi isiyo ya Kiserikali TUWODO inayoshughulika na shughuli za kijamii Wilayani Ilala.
“”SHIRIKA la TUWODO linajivunia mafanikio katika nyanja mbali mbali ikiwemo kuwainua wanawake kiuchumi na wanaofanya biashara ndogo ndogo ambapo TUWODO iliwatambua na kuendesha makongamano ili wajasiriamali Wanawake waweze kutambua fursa zilizopo Serikalini “alisema Awena
Mkurugenzi Awena Omary , alisema mafanikio mengine waliopata kuweza kupatiwa mafunzo mbali mbali ya kuweka akiba ,kukuza mitaji ,elimu ya biashara na masoko, umuhimu wa kutumia nishati safi katika kuleta maendeleo ya Taifa kwa ujumla ili waache kutumia matumizi mabaya ya kutumia kuni na mkaa ambao unachangia uharibifu wa mazingira .
Alisema TUWODO ni shirika lisilo la kiserikali ambalo limesajiliwa kupitia Wizara ya maendeleo ya jamii jinsia watoto na makundi maalum ambapo mwaka 2002 walisajiliwa rasmi.
Aidha alisema TUWODO kwa kushirikiana na Wanawake Wajasiriamali wameamua kwa pamoja kuendesha Kongamano la siku moja ambapo litakuwa endelevu katika sehemu mbalimbali kwa lengo kuwapatia masuala ya urasimishaji na uchumi.
“Taasisi ya TUWODO kipekee wanamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto na Makundi Maalum pamoja na Ofisi ya Rais TAMISEMI, zimeweza kuweka jitihada kubwa kwa wanawake kupitia mfuko wa Halmashauri ya asilimia kumi “alisema
Alisema palipo na mafanikio hapakosi changamoto katika ofisi yetu tumekuwa tukikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa fedha ,na rasilimali vifaa kutokana na kukosa wafadhiri wa ndani na nje ya nchi ambapo mapato yao yanatokana na wanachama na wadau wa Maendeleo.
Awena Omary alisema changamoto nyingine wanaomba Serikali, Halmashauri ya jiji iwapatie majengo yaliopo wilayani Ilala ambayo hayatumiki yalio yalio chini ya Serikali ili waweze kuchangia gharama ndogo za umeme na maji ili waweze kufikia malengo yao.
Kwa upande wake mgeni rasmi Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Ilala Neema Kiusa ,ambaye alimwakirisha Mkuu wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, Neema alisema kuhusiana na changamoto za Ofisi za TUWODO anawasilisha kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, aweze kuwatafutia jengo la Ofisi .
More Stories
Waziri Lukuvi aeleza maono ya Isimani ijayo
Madiwani Korogwe TC wahakikishiwa maji ya uhakika
CHADEMA wampongeza Mkurugenzi Mpanda