January 9, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TAASISI ya Pure Earth ya kimarekani yawakutanisha wadau mbalimbali wa mazingira

Na David John, TimesMajira Online

TAASISI ya Pure Earth ya kimarekani ambayo inafanya kazi duniani kote ikiwamo Nchini Tanzania imewakutanisha wadau mbalimbali wa mazingira kwa lengo la kuangalia athari ambayo inaweza kujitokeza kutokana na uwepo wa betri chakavu pamoja na vifaa vya umeme vya kielectroniki.

Akizungumza katika warsha hiyo ya siku moja iliyofanyika Ndani ya halmashauri ya jijini la Dar es Salaam Jamali Baruti Meneja sheria kutoka Baraza la Kusimamia Mazingira ofisi ya Makamu wa Rais NEMC amesema kuwa warsha hiyo ni muhimu na imeweza kukutanisha wadau kutoka idara zote mbalimbali zinazohusu mazingira.

Amesema kuwa Pure Earth imeweza kuwakuitanisha kwa lengo la kuangalia matumizi sahihi ya betri ambazo zinakuwa na madini ya risasi na athari zake na kwamba huko nyuma walikutana na waliweza kutoa mapendekezo ya kisera pamoja na mikakati ya namna gani kusimamia hizo betri zenye acid tindikali na masuala mazima ya kulinda mazingira.

“Ndugu zangu hapa kuna wajibu wa mzalishaji au mwagizaji kusimamia kuanzia zinakotoka hadi kuingizwa na zinavyotumika kwa uzuri na kwamba pamoja na yote lakini kuna changamoto ya taka za kieletroniki hivyo serikali chini ya ofisi ya makamu wa rais wamepitsha kanuni za usimamizi wa taka” alisema.

Nakuongeza kuwa ” kanuni hizi ndani yake kuna wajibu wa mzalishaji kupitia kanuni ya 52 inatoa maelekezo kwa waagizaji au wazalishaji kuwa taka hizo zinasagwa na zinahifadhiwa vizuri kwa ajili ya kuteketezwa ili kulinda mazingira lakini pia kuazisha mifumo ya ukusanyaji bidhaa taka hizi na hapa tutahakikisha sheria zinafanya kazi.

Akizungumzia ukusanyaji taka usio rasmi huko mitaani .Baruti alisema watu hao wapo na kimsingi wanajua kuwa kufanya biashara ya chuma chakavu au betri bila kuwa na kibalri ni makosa ila wao wamejipanga kukuza uelewa kwa lengo la kuwafanya kujua madhara ya maji ya betri na kusimamia kanuni..

Kwa upande wake mratibu kutoka taasisi hiyo ya Ppure Eearth hapa nchini Abdallah Mkindi alisema utafiti uliofanyika juu ya usimamizi wa vitu betri chakavu haujitoshelezi hivyo kutokana na hali hiyo ulipelekea kuandaa mapendekezo ya kisera , mpango mkakati wa usimamizi.

Alisema Moja ya mapendekezo waliyokubaliana nikuazisha sheria ambayo itaongeza jukumu la kusimamia betri chakavu kwa mzalishaji au muagizaji toka nje hivyo mkutano huo uliowakutanisha wadau ulilenga namna gani betri chakavu inalindwa zinasimamiwa ili kutunza mazingira na afya yza binadamu hivyo kikao kilikuwa na manufaa mengi kwani kinawezesha serikali badala ya yenyewe kubeba mzigo kuhusu chuma betry chakavu basi wazaliishaji au waingizaji nao pia wanapaswa kusimamia .

Pia alisema katika eneo hilo serikali inapaswa kuweka Sera na sheria ili kuwabana wanaozalisha au kuagiza kuhakikisha gharama pia zinatolewa na wenyewe na si kuiachia serikali peke yake.

Kwa upande wa washiriki kutoka halmashuri zote za jiji la Dar es Salaam akiwamo Pphina Benard kutoka Ttemeke na mjasirliamli Dominiko Kisika kutoka taasisi ya Nangasu Kkimara Mmbezi walisema warsha hiyo imewasaidia kupata uelewa mkubwa juu ya athari za betri chakavu na vifaa vya kielectroniki hivyo wametumia mkutano huo na wenyewe kwenda kutoa elimu ambayo wameipata hususani dhana zima ya uihifadhi wa mazingira