Na Jackline Martin, TimesMajira Online, Dar es Salaam
TAASISI isiyo ya Kiserikali MyLEGACY imekutana na kufanya mazungumzo na wadau kutoka makundi mbalimbali kwa ajili ya kuangalia haki za wanawake, vijana na watu wenye Ulemavu katika suala zima la upatikanaji wa ardhi.
Lengo la hatua hiyo ni kuweza kushirikiana na wadau wengine kwenye kuangalia
haki za makundi hayo kama sehemu ya kutekeleza mradi wao wa kuboresha maeneo ya makazi pamoja na kujifunzia.
Akizungumza wakati wa kikao hicho ambacho kilianza Desemba juzi
na kutarajiwa kumalizika leo, mwaka huu, Mkurugenzi Mtendaji wa My Legacy , Fortunata Temu amesema katika mkutano huo walifanya mapitio ya tafiti mbalimbali
ambazo zimefanyika kuweza kubaini changamoto ambazo vijana, wanawake na watu wenye Ulemavu wanazipata katika kutafuta haki ya kumiliki ardhi na mali nyingine.
“Tunawashirikisha wadau kuhusu mapitio hayo na tuna mpango wa kufanya uchechemuzi ili kuweza kuboresha changamoto ambazo zimeonekana,”
Amezitaja changamoto kadhaa ambazo wamezibaini ambapo amesema moja
ya changamoto hizo ni upatikanaji wa ardhi ambapo mara nyingi kinachotumika
kuamua ni sheria za mila na hasa katika masuala ya urithi wa ardhi kama mali
ambapo mila nyingi na desturi zinawabagua wanawake.
Pia amesema watu wenye Ulemavu kutokana na hali zao, mtizamo na fikra za
jamii wanaonekana kama wategemezi ambapo hawapewi kipaumbele katika
kupewa haki za ardhi.
Amesema hiyo ni kutokana na mitizamo potofu au fikra ambazo hazisaidii katika
kuwawezesha makundi hayo ili kujiona yana haki sawa ya kumiliki ardhi.
Kwa upande wa changamoto za wanawake, Temu amesema; “Wanawake katika upande wa mirathi pamoja
na mchango wao mkubwa hakuna kipaumbele kikubwa watapewa.”
Kwa upande wake mwakilishi kutoka Tasisi
ya Mawakili Vijana, Rojas Fungo amepongeza jitihada za My Legacy na hatua waliyochukua kushirikisha
wadau mbalimbali ili wawe sehemu ya mchakato wa kuhakikisha kwamba
wanafanya uchechemuzi ya kuhakikisha makundi hayo tajwa yanapata haki yao ya
msingi ya kumiliki ardhi.
“Ardhi ni suala muhimu sana kwenye maisha ya binadamu, kwa sababu watu wanaitumia kufanya shughuli za kiuchumi,
kilimo, hivyo ni nyenzo muhimu katika maisha ya binadamu.
“ Tunatamani kuona wanawake, vijana na wenzetu wanaoishi na Ulemavu wanapata haki hii ya msingi ya kumiliki kwenye maeneo yao, aidha kwa kurithi,kununua, au
kugawiwa na Serikali”
Naye mwakilishi wa watu wenye Ulemavu, Yahaya Bilali ameiomba serikali iweze kuwapatia Mabalozi wachini ili waweze kupata haki zao zote za msingi kwa wakati ambazo zimekua zinasahaulika kwani wamekua na changamoto nyingi ikiwemo umiliki wa ardhi na vitu vingine ambavyo serikali wamekua wakitoa kwaajili ya watu wenye ulemavu.
Aidha ameiomba serikali kuwakumbuka katika mikopo ambayo wamekua wakiitoa ya asilimia 2 kwa walemavu kuhakikisha wanaipata kwa wakati kwa kuwawekea wawakilishi ambao watakua wanafatilia kwa wakati.
More Stories
AZAKI yawasilisha mapendekezo yao kwa Serikali katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050
CP.Wakilyamba :Uvamizi maeneo ya hifadhi ya taifa katavi haukubaliki
Watu wawili wanaodhaniwa majambazi wapigwa risasi na Polisi