December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete yawasogezea huduma wananchi mkoani Geita yawaita kupata huduma zao.

Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo Dkt Salehe Mwinchete

Na David John Timesmajiraonline Geita

TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imeleta kliniki ya maalum”V.I.P” ya huduma ya magonjwa ya moyo,Kliniki ambayo inapatikana katika maonyesho ya sita(6) ya teknolojia ya madini yanayofanyika mkoani Geita .

Akizungumza na waandishi wa habari septemba 23 mwaka huu kwenye viwanja vya maonyesho hayo ambayo yanafanyika kwenye viwanja vya EPZA Bombambili Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo Dkt Salehe Mwinchete amesema kuwa wamelazimika kuwa sogezea huduma wananchi wa Kanda ya ziwa.

Amesema kuwa wao kama Taasisi ya Jakaya wamejipanga vizuri Kwa lengo la kuwahudumia watanzania na Kwa kupitia maonyesho ya teknolojia ya madini ambayo yanafanyika mkoani Geita hivyo wananchi wajitokeze kwenye Banda lao la Taasisi ya Jakaya kIkwete ili kupata huduma sahihi.

“Leo tumeleta katika maonyesho ya madini hii kliniki maalum inaitwa V.I.P kliniki ambayo ni ya watu mashauri lakini kwetu sio watu mashuhuri wenye pesa hii kliniki ni kwa kila mtu mwenye uhitaji wa huduma hii” Amesema

Kuhusu kutoa huduma Kwa kliniki hiyo Dkt Salehe Amesema Mtu ataomba siku na muda ambayo anataka kuja kuhudumiwa katika kliniki maalum, nakwamba atakutana na mazingira mazuri ya huduma.

“Tutamfanyia huduma zote hapa hapa alipo kwa maana atamuona daktari ,atapata vipimo na pia atapatiwa kiburudisho cha chai akiwa anasubiria majibu”Amesema Dkt Salehe

Pia Dkt Salehe ameelezea vyanzo tofauti tofauti vya maradhi ya moyo alisema kuwa ni ulevi,uvutaji wa sigara,matumizi ya chumvi nyingi katika chakula hivyo ameitaka na kuhihasa jamii kupunguza matumizi ya sigara na pombe ili kuepukana na maradhi ya moyo.