January 5, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Taasisi ya HakiElimu yaadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwake

Na Jackline Martin, TimesMajira,Online

Taasisi ya HakiElimu katika kuadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwake imezindua mpango mkakati wa miaka mitano ijayo yaani 2022-2026 ambao umeshirikisha wadau mbalimbali ikiwemo serikali na wajumbe wa bodi wenye lengo la kuendelea kuboresha sekta ya elimu nchini.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mkurugenzi wa HakiElimu Dkt. John Kalage amesema mafanikio ya HakiElimu ni kutokana na juhudi za pamoja na ushirikiano mahiri;

“Nia na juhudi za pamoja ndiyo zilipelekea taaisis ya HakiElimu kuwa na mafanikio na hata kuendelea kupanga mikakati ya baada ya miaka 20”

Aidha amesema pasipo mchango wa wadau wa elimu safari ya miaka 20 ya HakiElimu ingekua na historia nyingine;

“Wadau wa elimu mmekuwa nguzo muhimu sana ya safari hii ya miaka 20 ya HakiElimu kwahakika pasipo mchango wenu na hasa kwa kitaalamu na kifedha, safari ingekuwa na historia nyingine”

Pia amesema aliwashukuru wadau kwa ujumla , wananchi, walimu, wanafunzi, marafiki wa elimu, Asasi za kiraia, Taasisi za kifedha na Biashara, watoa huduma, waandishi wa habari kwa kuwa nguzo, pamoja na kufanya kazi kwamba wamekuwa pamoja sehemu ya nguvu kazi kwa kipindi chote Cha miaka 20 ya Hakielimu.

Ameongeza kuwa Safari yetu hiyo ya miaka 20 ya HakiElimu ilikua na mambo mengi hivyo wasingeweza kufika hapo bila ushirikiano wa serikali, wadau wa maendeleo, marafiki wa elimu, wananchi katika sekta mbalimbali na viongozi kwa ujumla waliopo katika sekta ya elimu.

Naye Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Prof. Carolyne Nombo alisema wapo tayari kushirikiana na Asasi za kiraia katika kuleta maendeleo kwenye sekta ya elimu lakini pia kwenye sekta mbalimbali.

Mbali na hayo alisema kuwa kwa sasa serikali wamefungua mjadala juu ya sera ya elimu na mitaala;

“Natambua kwamba wote ambao ni wadau wa elimu wanafahamu kwamba serikali yetu kupitia Wizara ya elimu tumefungua mjadala juu ya sera ya elimu na mitaala tukitambua kuwa elimu ni mali ya watanzania na siyo ya Wizara ya elimu”

Naye Mwenyekiti wa Bodi, Mwanachama Muanzilishi na Mwandishi wa vitabu Mabala Makengeza amesema Hakielimu haina lengo la kubomoa utafiti wa serikali hivyo daima wametumia sana utafiti wa serikali, takwimu na nyaraka za serikali katika kuonesha mambo ambayo bado yanahitajika kufanyika na kutumia ubunifu wao katika kuhakikisha suala hilo linafanikiwa.

T