Na Herishaban, TimesMajira Online, Ilala
TAASISI ya Fahari Tuamke Maendeleo iliyopo wilayani Ilala imetoa msaada wa vyakula na vifaa vya shule kwa wanafunzi wa mahitaji Maalum wa shule ya Msingi Mzambarauni Jimbo la Ukonga .
Msaada huo ulitolewa na Mkurugenzi wa shule ya Fahari Day Care Neema Mchau ,kwa wanafunzi wa shule hiyo ili waweze kutumia kwani na wao ni sehemu ya jamii .
“Taasisi yetu ya Fahari imeweka utaratibu wake endelevu ambapo kila mwaka kutoa msaada kwa jamii ya mahitaji maalum misaada hii tunawashirisha Wazazi wa wanafunzi wa shule yetu “alisema Neema
Mkurugenzi wa Fahari Tuamke Maendeleo Neema Mchau ,alisema msaada huo waliotoa wa vyakula ni endelevu kila mwaka kusaidia jamii kwa kushirikiana na Wazazi wa wanafunzi wa watoto wanaosoma shule ya Fahari Day Care dhumuni kuwajengea upendo watoto wa mazingira magumu wakue katika msingi bora .
Alisema katika ziara hiyo shule ya msingi Mzambarauni wametoa vyakula mbali mbali ikiwemo mchele,sukari,maharage, unga na vifaa vya shule daftari ,peni sabuni ,Taulo za kike,
Taasisi ya Fahari Tuamke Maendeleo iliyopo wilayani Ilala kata Gongolamboto inamiliki kituo cha watoto, wa Day Care ambapo ipo matari wa mbele kuunga mkono juhudi za Serikali katika sera ya elimu bure .
Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Mzambarauni Maria Thomas Liyombo, alisema wanafunzi wa mahitaji maalum idadi yao 150 ambao wanasoma shule hiyo.
Mwalimu Maria Thomas Liyombo, alisema kila mwaka wanafunzi hao wa ,Kitengo maalum kitaaluma wanafanya vizuri katika masomo yao wameishauri Serikali kuongeza idadi ya walimu wa mahitaji Maalum.
Kwa upande wake Vivian Ugulumu kutoka (VIWOTA) alisema watoto viziwi wana uwezo wa kufanya mambo yote ambayo watoto wengine sio viziwi wanafanya hivyo ameishauri jamii kuongeza ulinzi kwa watoto wenye ulemavu sababu watu wengi utumia udhaifu wao.
Vivian alisema lengo kubwa la kuwajengea upendo na uwezo wawe wajasiri wa kuvunja ukimya pindi wanapofanyiwa vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia .
Alisema mtoto kiziwi anajengewa uwezo kwa ajili ya kuvunja ukimya akifanyiwa vitendo vya ukatili anakuwa na uwezo mkubwa kutoa ushahidi pindi anapofanyiwa vitendo vibaya.
More Stories
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini
Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi watakiwa kusimamia programu za chakula shuleni
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano