Na Mwandishi wetu,
Tarehe 03.03.2022 muda wa 01:00 jioni huko maeneo ya Esso kata ya unga limited katika halmashauri ya jiji la Arusha, gari lenye namba za usajili T.716 DRG aina Toyota Coaster iliyokuwa ikiendeshwa na ANORD KIMARO (39) mkazi wa mianzini iliungua moto na kusababisha kifo cha mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la GODFREY KESSY (30) utingo wa gari hiyo na mkazi wa Esso.
Ajali hiyo imetokea mara baada ya kuwashusha abiria waliokuwa wanatokea Mkoa wa Kilimanjaro kwaajili ya mazishi na walipofika maeneo ya Esso ghafla gari hilo liliwaka moto na kuteketea pamoja na utingo wa
gari hilo ambae alishindwa kutoka na kusababisha kuungua akiwa ndani ya gari hilo Aidha dereva wa gari hilo yeye alifanikiwa kuvunja kioo cha mbele na kufanikiwa kutoka huku akiwa na majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake.
Uchunguzi wa Jeshi la Polisi Mkoani hapa umebaini kuwa chanzo cha ajali hiyo ni itilafu ya mfumo wa umeme kitendo kilichosababisha kuungua kwa gari hilo. Pia majeruhi katika ajali hiyo anaendelea kupatiwa katika hospitali ya kaloleni.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa Mount Meru jijini Arusha kwa uchunguzi wa kidaktari.
Nitoe wito kwa wamiliki wa vyombo vya moto kufanya matengenezo na uchunguzi wa mara kwa mara wa vyombo vyao ili kuepusha madhara makubwa yanayoweza kutokea.Pia niwaombe wamiliki na watumiaji wa vyombo vya moto kutumia muda huu uliotolewa na Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani kuyafikisha magari yao katika kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Arusha kukagua magaria yao.
IMETOLEWA NA:
JUSTINE MASEJO-ACP
KAMANDA WA POLISI
MKOA WA ARUSHA
More Stories
Tanzania,Uturuki kushirikiana kuinua sekta ya utalii nchini
Wanaoficha watoto wenye ulemavu kusakwa
Mawakili Tabora walaani kuziwa kutekeleza majukumu