June 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Swissport yatarajia kutoa Bil 1.8 kwa wanahisa wake

Na Mwandishi wetu, Timesmajira

KAMPUNI ya Usafirishaji mizingo (Swissport) inatarajia kutoa billioni 1.8 kwa wanahisa wake kama sehemu ya gawio .

Hayo yamebainishwa Jijini Dar es salaam mapema leo Juni 14, 2924 na Mkurugenzi Mkuu wa swissport Mrisho Yassin wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Mkutano 39 wa wanahisa wa Kampuni hiyo.

Amesema gawio hilo litamuzesha kila mwanahisa kupata shilingi 51.33 kama faida ambayo Kampuni hiyo imetegeneza kwa mwaka 2023.

“Faida ya Kampuni kwa mwaka 2023 ilikuwa billioni 3.6 kwa wanahisa wanaopewa asilimia 50 ya faida ambayo Kampuni imetegeneza kwa mwaka huu ukilinganishwa na mwaka 2022 ambapo ilipata billioni 2.6.”alisema Mrisho

Kwa upande wa gawio mrisho amesema mwaka 2022 kampuni ilitoa shilingi 41 kwa hisa Moja huku mwaka 2023 ikitoa gawio la shilingi 51.3 Kwa hisa ambayo ni ukuaji wa takribani asilimia 27 .

Amesema kupitia Filamu ya Royal tour imeweza kuchagia watu wengi kuja nchini Tanzania na kupelekea kukua kwa utalii

“Mapato ya Kampuni yameongezeka kulingana na ongezeko la huduma na shughuli mbalimbali ambazo tumekuwa tukizitoa”amesema mrisho

Aidha amesema miluko ya ndege kwa mwaka 2023 imeongezeka na kupelekea idadi ya mizingo kuongezeka jambo ambalo limeongeza mapato ya Kampuni hiyo

Naye mwanahisa wa kampuni hiyo, Aika Shauri amesema mkutano huo umekwenda vizuri na wanashukuru kwa gawio waliolipata na wanaona kampuni hiyo inaendelea kukua.

Irene Tarimo ambaye pia ni mwanahisa wa muda mrefu wa kampuni hiyo amasema Swissport inafanya vizuri hasa ya kuwasaidia wanachama wake kuweza kujikwamua kiuchumi.

“Wale ambao wanaweza kuja kuwekeza kama Swissport inavyofanya basi wasisite wafanye hivyo ili kuweza kuwasaidia watanzania kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umaskini,” amesema.