Na Mwandishi wetu,Timesmajira
SWAHILI Fashion Week yaendelea kufanya vizuri zaidi huku washindi 27 wameibuka kidedea katika Tuzo na kutambuliwa kwa mchango wao bora katika sekta ya mitindo tangu kuanzishwa kwake mwaka 2008.
Miongoni mwa washindi hao wa Swahili Fashion Week & Awards 2025 ni pamoja na
Hair Stylist of the Year kuyokakwa Dema,Make Up Artist of the Year kutoka kwa Jojo, Female Model of the Year ni Zulfa Yazid,Male Model of the Year ni Kami, 361 Degrees Designer of the Year ni ÿMac Couture; Fashion Entrepreneur of the Year nin Anna Collections Fashion Academy.
Wengine ni Khimji’s Menswear Designer of the Year ni JM International.),Fashion Photographer of the Year( Dadpixel;) ni Gen-Z Stylish, Personality of the Year ni Prisca Lymo; Male Stylish Personality of the Year ni Mc Nsena; Female Stylish Personality of the Year ni Jasinta Makwabe; Womenswear Designer of the Year ni Michael Williams; Accessory Designer of the Year ni Bella Ragazza; Onomo Hotel Designer of the Year (Mikoani) ni Irene Designs TZ (Dodoma); Costume Design in Film/Series of the Year ni Kombolela; Hugo Domingo Stylist of the Year ni Rada Designer,Fashion Content Creator of the Year ni Gaza Boe; Stylish Music Video of the Year ni Jux ft Diamond (Ololufe Mi); Fashion Journalist of the Year ni Betty Boniface Omara (Azam TV); Innovative Designer of the Year ni Rada Designer; Fashion Modesty Designer of the Year ni Her Modesty; Khimji’s Upcoming Designer of the Year ni Gazelle Couture; Washington Benbella Emerging Designer of the Year ni Smart Kiss; Hon. Zakhia Meghji Lifetime Achievement Award ni Jamila Vera Swai; New Face of the Year ni Naomi Kaaya; Humanitarian of the Year ni Mama Jasiri; Runway Moment of the Year ni Naisae Yona (Miss Universe Tanzania).

Taarifa iliyotolewa kwa waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam na Mwanzilishi na Mmiliki wa Swahili Fashion Week & Awards
Mustafa Hassanali, alisema dira yao daima imekuwa kuinua mitindo ya Kiafrika kufikia viwango vya kimataifa huku wakienzi utambulisho wao wa kipekee wa
Alisema Swahili Fashion Week imendelea kuwa taa ya ubunifu, uvumbuzi na fursa kwa wabunifu barani Afrika na katika diaspora.
” Imebaki kuwa nguzo muhimu kwa wabunifu kutoka nchi zinazozungumza Kiswahili na zaidi ya hapo, kuwapa nafasi ya kuonyesha kazi zao, kuunganika na wadau wa tasnia, na kupata masoko ya kimataifaikiendeleza simulizi la “Made in Africa” lenye mizizi ya urithi na uwasilishaji wa kisasa.
“Kuendeleza Vipaji Vipya Shindano la Washington Benbella Emerging Designers Competition (WBEDC) limeendelea kuwa ngazi kwa vipaji vipya nchini Tanzania na barani Afrika. Mwaka huu, jukwaa hili liliendelea kuibua nyota wapya, ikiendeleza mafanikio ya waliowahi kung’ara kama Philista Oniang’o (Kenya, 2012), na wengine wengi waliopanda chati za mafanikio sekta ya mitindo,”amesisitiza

Aidha amesema uwezeshaji wa Kibiashara kwani itakusaidia ushirikiano na wadau muhimu, ikiwemo taasisi za kifedha huku Swahili Fashion Week iliendeleza mafunzo ya umahiri wa kifedha na ujasiriamali kwa wabunifu.
“Mwaka huu, kwa kushirikiana kwa karibu na CRDB Bank Plc benki kubwa zaidi ya kibiashara nchini Tanzania kupitia Tanzania Fashion Forum, tulijikita katika kujenga uelewa wa kifedha kwa jamii ya mitindo ili kuwasaidia kusimamia, kukuza, na kudumisha biashara zao za ubunifu.

More Stories
Dkt.Tulia,Mwalunenge waungana kutatua changamoto ya barabara
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi
Kihongosi:Uhai wa chama mashina