Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
MKUU wa benchi la Ufundi la klabu ya Simba, Sven Vandenbroeck ametaka mtu yeyote iwe ndani ya klabu, nje, wapenzi na hata mashabiki kuwakosoa wachezaji wake ambao wamekuwa wakijitoa kwa kila hali ya ajili ya timu yao.
Sven amewajia juu baada ya baadhi ya watu kukosoa ushindi wao wa goli 5-0 walioupata katika mchezo wao wa juzi wa Kombe la Shirikisho la la Azam ‘Azam Sports Federation Cup (ASFC)’ dhidi ya Majimaji FC ya Songea na kufanikiwa kutinga hatua ya nne ya mashindano hayo.
Katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Mkapa, magoli ya Simba yalifungwa na beki Gadiel Michael, Chris Mugalu, Ibrahim Ame, Meddie Kagere na Luis Miquissone huku kocha huyo akiweka wazi kuwa timu hiyo imewapa mchezo mzuri ambao wanauchukulia kama wa kirafiki waliopaswa kucheza na ndio maana kikosi chake kilikuwa na mabadiliko makubwa ya wachezaji.
Kocha huyo amesema, toka dakika kwanza wachezaji wake walionesha kuwa walikuwa wakihitaji zaidi ushindi jambo ambalo ni zuri kwani unapokuwa na kikosi ambacho kila mchezaji anaonesha uwezo inakuwa rahisi kufikia malengo.
Amesema kuwa, baada ya kupata goli hizo na kushindwa kufikia rekodi ya mwaka jana ambapo waliifunga timu ya Arusha goli 6-0, watu wengi wameanza kuikosoa timu kuwa magoli wanayofunga hayatoshi.
Sven amesema, toka walipokuwa Nigeria karibu wachezaji wake wote waliumwa na hadi sasa wapo wapo wanaoumwa lakini wanajitoa kwa ajili ya klabu na jezi yao hivyo ameomba mtu yeyote yule asitokee akawakosoa wachezaji wake ambao wamejitoa kufa na kupona kwa ajili ya klabu.
“Badala ya kukaa na kuwakosoa wachezaji wangu ni vema mkazungumza kuhusu mimi, naomba muwaache wachezaji wangu ambao kila siku wamekuwa wakijitoa kwa asilimia 100 hata pale am bapo hawajisikii vizuri, ” amesema kocha huyo.
More Stories
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes
Rais Samia: Yanga endeleeni kuipeperusha bendera ya Tanzania