PHOENIX, Arizona
TIMU ya Kikapu ya Phoenix Suns imefanikiwa kuibuka na ushindi wa vikapu 118-108 dhidi ya Milwaukee Bucks katika mchezo wa fainali ya kwanza ya Ligi Kuu ya Kikapu nchini Marekani NBA, iliyochezwa usiku wa kuamkia leo na kuongoza Kwa alama 2-0.
Katika mchezo huo nyota wa Suns Devin Booker, aliifungia timu yake alama 31, huku Paul akiiongeza alama 23 kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.
Akizungumza mara baada ya mchezo huo nyota wa Suns, Devin Booker amesema waliutafakari sana mchezo huo kabla ya kuingia uwanjani kwani walipanga kufanya kweli ili kuibuka na ushindi.
Kwa upande wa Bucks nyota wa timu hiyo Antetokounmpo aliifungi timu yake alama 42 na marudio 12, huu ulikuwa mchezo wa pili kwake baada ya kukosa michezo miwili kwa sababu ya kusumbuliwa na jeraha la goti la kushoto.
Tayari timu ya Suns inaongoza alama 2-0 huku walijiandaa kwenda Milwaukee timu ambayo inacheza fainali kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1974.
More Stories
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes
Rais Samia: Yanga endeleeni kuipeperusha bendera ya Tanzania