Na Bakari Lulela,TimesMajira Online
BENKI ya Stanbic imezindua kampeni maalumu ya Stanbic madawati initiative yenye lengo la kuendeleza na kuinua sekta ya elimu nchini ambapo imeikabidhi serikali jumla ya madawati yapatayo 2000.
Akizungumza Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ufundi,Prof. Joyce Ndalichako ameipongeza benki hiyo kwa kuonyesha uzalendo wa kweli wa kuwekeza kwa minajili ya kuwasaidia Watanzania kupata elimu bora.
“Serikali inatambua mchango wenu hivyo tunawapongeza kwa kuanzisha kampeni hii ya Stanbic madawati initiatives yenye lengo la kuisaida jamii katika upatikanaji wa elimu bora shuleni,” amesema Prof.Ndalichako
Prof. Ndalichako ameeleza kuwa pamoja na uzinduaji wa kampeni hiyo Stanbic benki imekuwa ni msaada mkubwa kwa wananchi ambapo ameweza kuchangia kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni moja kwa ajili ya kuisaidia jamii.
Hata hivyo Waziri huyo amesema kwamba elimu ni mhimili mkubwa katika maisha ya mwanadamu hivyo faifa lolote haliwezi kupata maendeleo katika uwekezaji bila ya kuwa na elimu.
Aidha Profesa Ndalichako amesema kwamba ndoto za maendeleo zitafanikiwa kama kutakuwa na ushirikiano mzuri baina yetu na elimu ndio msingi wa maisha hivyo ni vema kuhakikisha vijana wetu wanaipata.
Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha biashara wa benki hiyo Omari Ntiga amesema benki yao imekuwa ikishiriki katika mipango mbalimbali ya kuisaidia jamii hususan katika sekta ya elimu, kilimo pamoja na utoaji wa huduma za bima za afya kwa wananchi.
Hata hivyo benki ya Stanbic imekuwa na utaratibu wa kutoa ajira kwa vijana wa kitanzania wanaokuwa wakihitimu kutoka vyuo vikuu.
More Stories
Kongamano la Uwekezaji kati ya Tanzania na Ubelgiji lafanyika Dar
CCM kuhitimisha kampeni kwa kishindo
Walimu elimu ya lazima watatakiwa kuwa wabobezi kwenye masomo wanayofundisha