November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

STAMICO yaongeza mapato ya ndani hadi bil. 61.1/-

Na Jackline Martin, TimesMajira Online

SHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO)
limefanikiwa kuongezeka kwa mapato ya ndani kutoka sh. Bilioni 1.3 kwa Mwaka 2018/19 hadi sh. Bilioni 61.1 kwa mwaka 2022/23
ambalo ni ongezeko la asilimia zaidi ya 4,425

Kwa miaka mitatu iliyopita Shirika lilikuwa
linakusanya kutoka vyanzo vya ndani sh.
Bilioni 1.3 kwa mwaka, ambapo wakati huo
huo lilikuwa linachukua ruzuku sh. Bilioni 3.4.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mtendaji
wa STAMICO, Dkt. Venance Mwasse, wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari, jana Jijini Dar es Salaam kuhusu utekelezaji wa shughuli za shirika hilo.

Dkt. Mwasse alisema tangu kuanzishwa kwa shirika mwaka 1972, halikuwahi kupeleka kitu chochote serikalini, ambapo kwa sasa tangu wapate mafanikio shirika limefanikiwa kulipa gawio serikalini sh.Bilioni 8.

Aidha Dkt. Mwasse alisema shirika
limefanikiwa kupata hati safi kwa miaka 3
mfululizo kutokana na ukaguzi wa mahesabu.

Pia alisema wamefanikiwa kupata kandarasi za uchorongaji, ambapo kwa mwaka huu Aprili wamefanikiwa kusaini mkataba wenye thamani ya sh. Bilioni 55.2


Pia Dkt. Mwasse alisema pamoja na kulipa gawio na kuhudumia makundi maalumu, kwa mwaka huu wamefanikiwa kuwekeza kwenye miradi yao kwa kiasi cha sh. Bilioni 17.8

Mbali na hayo Dkt. Mwasse alisema
wamefanikiwa kupata leseni mpya 6 zikiwemo 4 za madini ya Kimkakati za lithium, Graphite, REE na Copper.

Kuhusu mipango yake ya baadae, Dkt. Mwasse alisema shirika hilo limejipanga Kuimarisha uchimbaji mkubwa wa makaa ya mawe, kuongeza uwekezaji wake kwenye tasnia ya uchorongaji, kuendeleza leseni za Shirika na kuzitangaza kwa lengo la kupata wawekezaji wa madini ya ya kimkakati