NA
K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, MBEYA
SPIKA
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb),
ametembelea banda la Mfuko wa Fidia kwa wafanyakazi (WCF) kwenye Maonesho ya
Kimataifa ya Kilimo Tanzania kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya
leo Agosti 4, 2023.
Mhe.
Dkt. Ackson ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, alipata fursa ya
kupewa elimu ya Fidia kwa Wafanyakazi iliyokuwa ikitolewa na Afisa Mfawidhi
WCF, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Bi. Rose Satta.
Alijulishwa
kuwa WCF inatoa fidia endapo mfanyakazi ataumia au kuugua kutokana na kazi na
endapo atafariki basi wategemezi wake watalipwa fidia.
Pia
alielezwa kuwa Mfuko uliundwa kwa mujibu wa Kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia
kwa Wafanyakazi [Sura 263 marejeo ya mwaka 2015] na inahusu waajiri na
waajiriwa wote kutoka sekta ya umma na binafsi Tanzania Bara.
Aidha
Mhe, Spika alielezwa kuwa Mfuko unatoa jumla ya Mafao saba ambayo ni pamoja na Huduma
ya matibabu, Malipo ya ulemavu wa muda, Malipo ya ulemavu wa kudumu, Malipo kwa
anayemhudumia mgonjwa, Huduma za utengemao, Msaada wa mazishi na Malipo kwa
wategemezi endapo mfanyakazi atafariki.
Maonesho
ya mwaka huu ambayo yalifunguliwa rasmi Agosti Mosi, 2023 na Makamu wa Rais,
Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, yamewaleta pamoja washiriki kutoka nchi
zinazofikia 30, kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Homera na
yamebeba kaulimbiu isemayo “Vijana na
Wanawake ni Msingi Imara wa Mfumo Endelevu wa Chakula”
More Stories
Zaidi ya wananchi 32,000 Vijiji vya Wilaya za Morogoro na Mvomero kuanza kupata mawasiliano
Wafanyabiashara waomba elimu ya namna watakavyorejea soko kuu
DCEA,Vyombo vya Ulinzi na Usalama vyafanya operesheni ya kihistoria