December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Spika Tulia afungua kikao cha Bunge la 12 Mkutano wa 7

Na Amida Jamal, TimesMajira Online

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson amefungua Kikao cha Bunge la 12 Mkutano wa 7 wa Bunge la Bajeti April 5, 2022 Dodoma.

Katika kikao hicho Dkt. Tulia ackson ameongoza mkutano huo ambapo wabunge wameuliza maswari katika sekta mbalimbali.

Naye mbunge wa viti maalumu la Tanzania Halima James Mdee aliuliza swari kupitia sekta ya ujenzi na uchukuzi ambapo aliitaka serikali iwe wazi kuelezea kiundani zaidi mipango ya bajeti mwaka 2022.

“Serikali kupitia sekta ya ujenzi na uchukuzi mwaka 2021/2022 ilitenga fedha tilioni 1.5 ambapo bunge na ilipitisha na machi 2022 ilitoa tilioni 1.0 lakini miradi mingi haijajengwa na fedha hiyo imelipa madeni” Amesema Halima mdee.

Waziri wa Fedha na Mipango Mwigulu mchemba alijibu swari la halima mdee kwa kusema serikali haiwezi kulipa kama miradi haijakamilika hivyo kazi ifanyike ndio watu walipwe na sio kama madeni yakilipwa miradi mingine itasimama bali madeni yatalipwa huku miradi mingine ikiendelea kujengwa.

“Hakuna kazi ambayo inalipwa kabla haijakamilika kama tumeweza kujenga reli sidhani kama tutashindwa kujenga barabara” Amesema Mwigulu mchemba akijibu swari la halima mdee.

Spika wa bunge Dkt. Tulia ackson aliongeza kuwa baada ya mkutano wa bunge kumalizia wabunge wataelekea ukumbi wa msekwa ambapo kutakuwa na kikao cha kujadiri uchunguzi wa uchafuzi wa mto Mara na kusababisha kufa kwa samaki ambapo taarifa hiyo itawasilishwa na waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Rais muungano na Mazingira Dkt. Seleman Jafo.

Mkutano wa 7 wa bunge la 12 umeanza Rasmi April 5, 2022 na utaendelea ambapo kutokana na ratiba ya mwezi wa Ramadhani bunge litaanza saa 3 hadi saa 7 na saa 10 hadi saa 12.