Na Esther Macha, Timesmajira,Online,Rungwe
SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Dkt.Tulia Ackson amezindua Taasisi Suma Ikenda Foundation yenye lengo la kusaidia watu wenye mahitaji maalum
ambayo Mkurugenzi wake ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya Suma Ikenda Fyandomo.
Akizungumza katika hotuba yake Spika Dkt.Tulia amesema tukio hili ni la heri ambalo limeanzishwa na Mkurugenzi wake Suma Ikenda ambaye ni Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Mbeya hivyo kila mmoja anapaswa kulipongeza na kumuunga mkono kwa hali na mali.
Hata hivyo amesema kila mmoja anapaswa kumuunga mkono Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyotekekeza miradi mbalimbali ya maendeleo.
Amempongeza kwa kuhudumia sekta ya afya pia kuwajali watu wenye ulemavu.
Aidha alitoa wito kwa mkurugenzi wa Suma Ikenda Foundation kuwa na moyo kwa yale atakayoyafanya ili awe tayari kukabiliana na changamoto zitajazojitokeza wapo watajaoshukuru na wasioshukuru.
Yeye kama mdhamini wa Tulia Trust ameahidi kushirikiana na na Taasisi ya Suma Ikenda Foundation katika nyanja zote za kijamii.
Awali akisoma taarifa ya Taasisi,Timida Fyandomo amesema malengo ya kuanzishwa kwake ni kusaidia watu wenye mahitaji maalum.
Aliyataja makundi hayo kuwa ni pamoja na kufanya kazi na wanawake, wazee, vijana na watoto wa Mkoa wa Mbeya katika shughuli za ujasiliamali,kutafuta fursa, maslahi ya uchumi na kuwajengea uwezo wajasiliamali wanawake.
Suma Fyandomo amesema lengo la kuanzisha Taasisi yake ni kuisaidia jamii kama Wajasiriamali, Wanawake Wazee na Walemavu.
Kipekee amemshukuru Spika kwa uzinduzi wa Taasisi yake na kwamba kabla ya siasa kiu yake ni kuwasaidia wahitaji wakiwemo wahitaji sambamba na kuwasaidia wanawake na watoto na leo amefurahi kutimiza ndoto yake.
Ametoa mashine 12 za kukoboa na kusaga zenye thamani ya shilingi milioni sitini na nne,kitanda cha kujifungulia,viti mwendo vinne pia taulo za kike kwa wanafunzi na mashuka 50 ya hospitali.
Naye Mwenyekiti wa umoja wa wanawake (UWT) CCM Mkoa wa Mbeya Edina Mwaigomole ametoa wito kea wanufaika wa vifaa vilivyotolewa kuhakikisha wanatunza Ili viweze kuwaletea matunda mazuri.
Aidha Suma Ikenda Foundation imetoa tuzo kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Mashariki na Pwani Dkt Alex Malasusa amempongeza Fyandomo kwa kuanzisha Taasisi hiyo inayogusa jamii hivyo kama Kanisa linaunga mkono.
“Watanzania tusiichezee amani iliyopo kwani wenzetu hawana amani katika nchi zao hivi niletoka Congo kwenye maombi kuombea amani nchi hiyo hawana muda wa kufanya ibada”alisema Malasusa.
Katibu mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya Bashiru Madodi amesikitishwa na baadhi ya Wanambeya wanaosema Spika ajiuzuru kwa kupitisha hoja ya bandari bungeni.
“Itakuwa si busara kwa Wanambeya kujipinga wenyewe na hao wanaopinga wanayo maslahi binafsi na wataadhibiwa kwenye uchaguzi kwani wanatumia bandari kama kete ya siasa”amesema Madodi.
Mkuu wa Mkoa Juma Zuberi Homera amempongeza Fyandomo kwa kuizungumzia Mbeya na uanzishwaji wa Taasisi hiyo utaisaidia zaidi serikali.
Aidha amewapongeza Suma Ikenda Fyandomo na Bahati Ndingo kwa kuipigania Mbeya ikiwemo miradi ya Maji na miundombinu.
Hata hivyo amewataka wananchi kuchunga ndimi zao na kwamba mkataba wa bandari itashiriki wezi hivyo wanaopinga wanatetea wezi kwani baadhi ya Watanzania wanatumiwa na mabeberu na mahakamani haki itatendeka.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa