Na Doreen Aloyce,Dodoma
SPIKA wa Bunge Job Ndugai, amewataka wabunge wa CHADEMA wakiongozwa na Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe kurudisha pesa za wiki mbili ambazo ni zaidi ya sh. milioni 110 walizolipwa na Bunge.
Kauli hiyo ameitoa leo jioni wakati akiahirisha Bunge kufuatia barua ya Mbowe aliyoiandika wiki iliyopita ikiwataka wabunge wa CHADEMA kutokuudhuria Bunge kwa wiki mbili kuanzia Mei 1, mwaka huu ili kujiweka karantini.
Spika Ndugai amesema wabunge hao wakiongozwa na Mbowe walilipwa sh. milioni tatu na wengine sh. milioni 2.040,000 na baadaye kutokomea kusikojulikana.
Alisema kitendo hicho ni utoro wa hiari na alifananisha na wizi wa fedha za wananchi .
“Hicho kitendo mlichofanya ni cha kitapeli na wizi mkubwa. Kumbuka hizo ni pesa mlizolipwa ni za wananchi maskini ambao waliwaleta Bungeni kwa ajili ya kuwawakilisha kufanya kazi zao sasa nyie bila huruma mnaweka fedha mfukoni mnaondoka kwa kutoroka na migomo ambayo haina tija kwa jamiil,” alisema Ndugai.
More Stories
Wassira:Waliopora ardhi za vijiji warudishe kwa wananchi
Rais Samia apongezwa kwa miongozo madhubuti ya ukusanyaji wa kodi
Mwenda:Siku ya shukrani kwa mlipakodi ni maalum kwaajili ya kuwatambua,kuwashukuru