November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Somalia: Wanamgambo wa Al-Shabaab waua watu 10 na wengine kushambuliwa

Vikosi maalumu vya Somalia vinasema vimemaliza uvamizi Somali uliofanywa katika hoteli iliyopo katika mji mkuu Mogadishu ambayo ilivamiwa na wananamgambo wa al-Shabab Takriban watu 10 wameripotiwa kuuawa katika hoteli ya – Elite Hotel iliyopo katika eneo la ufukwe wa Lido, pamoja na wanamgambo kadhaa ambao idadi yao haijajulikana.

Washambuliaji walilipua bomu lililotegwa ndani ya gari nje ya hoteli hiyo Jumamosi usiku kabla ya kuivamia na kuwateka nyara watu.
Hoteli hiyo ambayo imejengwa hivi karibuni inamilikiwa na mbunge na ni maarufu kwa maafisa wa Somalia.

Walioshuhudia tukio hilo wanasema kwamaba mlipuko wa kwanza ulisikika kote mjini Mogadishu na kulikuwa na purukushani wakati watu walipokuwa wakitoroka kutoka eneo hilo.

Vikosi vya usalama viliizingira hoteli hiyo na kukabiliana kwa risasi na washambuliaji waliokuwa na silaha ndani ya hoteli. Saa nne baadae, msemaji wa serikali Ismael Mukhtaar Omar alituma ujumbe kwenye ukurasa wa Tweeter akisema kuwa uvamizi huo umekwisha na wavamizi wote wameuawa.

Haikuwa wazi mara moja ni wananamgambo wangapi walioshiriki shambulio hilo.

Gari la ambilansi likionekana katika Elite Hotel mjini Mogadishu, baada ya mlipuko
Miongoni mwa watu waliouawa ni pamoja na afisa wa ngazi ya juu kutoka wizara ya habari na afisa mwingine kutoka wizara ya ulinzi nchini humo. Makumi kadhaa zaidi wameripotiwa kujeruhiwa.

Wavuti wa shirika la habari la kibinafsi nchini Somalia Dhacdoone lilielezea hoteli hiyo kama moja ya maeneo yenye ulinzi mkali mjini Mogadishu.
Taarifa ya awali iliyotumwa kwenye mtandao ambayo ilidaiwa kutumwa na al-Shabab ilisema: “mujahideen wamefanya mashambulio yaliyofanywa na washambuliaji wa kujitolea muhanga kufa na makamanda na waliivamia hoteli ya mbunge wa serikali ya Somali.

Al-Shabab, ambayo ina uhusiano na kundi la al-Qaeda, wamekuwa wakiendesha mashambulizi ya ukatili nchini Somalia kwa zaidi ya muongo
Kundi hilo limesukumwa nje ya mji wa Mogadishu na wabajeshi wa serikali ya Somalia pamoja na Majeshi ya Muungano wa Afrika, lakini kundi hilo bado linafanya mashambuliya mabomu na mauaji katika mji huo mkuu.

Kwa kipindi cha miezi miwili mashambulio ya kundi hilo la Jihadi yameongezeka mjini Mogadishu.
Wiki iliyopita ufyatulianaji wa risasi baina ya wajumbe wa al shabab waliofungwa pamoja na maafisa wa usalama katika gereza yaliwauwa watu takriban.