November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Soko la kimataifa Feri kufanyiwa maboresho

Na Bakari Lulela, TimesMajira Online

IMEELEZWA kuwa miundombinu ya soko la kimataifa la samaki Feri jijini Dar es Salaam ipo kwenye hatua za maboresho katika baadhi ya maeneo Ili kuliweka katika muonekano mzuri wenye kuvutia watu wa kada mbalimbali . 

Akizungumza na mwandishi wetu meneja wa soko hilo mh.Selemani Mfinanga amesema maboresho hayo ni hatua ya moja wapo ya uboreshaji wa soko kimataifa Ili mazingira yawe rafiki kwa wafanyabiashara ambapo hivi sasa wamejenga mapaa kwenye zoni namba 2 na sehemu ya soko mjinga na maeneo ya kupumzikia wavuvi pindi watokapo baharini.

” Lengo ni kuyawezesha mazingira ya soko hilo kuwa rafiki kwa utoaji wa huduma bora zenye viwango maeneo mengine yatakayofanyiwa maboresho ni pamoja na  zoni namba 1 ,2 ,3 na 6 ambayo ni maalumu kwa kufanyia biashara  ya samaki na kwenye zoni namba 8A,” amesema Mfinanga

Meneja huyo ameeleza kwamba kwa nyakati tofauti  kutakuwa na maboresho yatakayo kuwa yakifanyika kuliweka soko katika hali nzuri ambapo kutakuwa na ujenzi wa maduka 28 yatakayokuwa karibu na kituo cha magari yaendayo kasi, yatayokuwa yakitoa huduma mbalimbali ikiwemo vifaa vya simu, mabucha ya samaki na Famasia Ili kuongeza mnyororo wa thamani

Aidha Mfinanga amesema kuwa hivi sasa baadhi  ya maeneo ya soko mafundi wapo site wakiendelea na kazi za uboreshaji wa miundombinu  ya msingi kama vile uwekaji wa marumaru na uondoaji wa maeneo korofi.

Hata hivyo  kutokana na vikao kazi walivyowahi kukaa na halmashauri  ya Jiji la Dar es salaam ambapo walionelea pawepo na  uwekezaji wa mradi wa uwekaji mitungi ya gesi aina ya ORXY wenye thamani ya sh. Million 300 ambao utakuwa ukisimamiwa na ORXY wenyewe.

Pia ameeleza kutakuwa na maboresho ya uwekaji wa majiko ya stamico ambayo ni nishati mbadala kwa watumiaji ambapo yatawasaidia mama,baba lishe kufanya shughuli za mapishi ya kuhudumia umma kwa mazingira safi na salama.

Sambamba na hayo wamebuni soko hilo kuliwekea picha ya samaki aina ya jodari ili iwe moja ya kivutio cha kipekee katika ukanda wa Afrika mashariki isitoshe kutakuwa na siku maalumu ya ‘samaki day’ ambapo watu wawe wanasherehekea kila mwaka.