December 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Snura afurahia kuvishwa kofia na Rais Magufuli

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

MSANII wa muziki miondoko ya Singeli hapa nchini Snura Mushi, amefurahia kuwa mwanamke wa kwanza kuvishwa kofia na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt John Magufuli.

Akizungumza mara baada ya kuvishwa kofia hiyo leo, kwenye Kampeni ya CCM iliyofanyika kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora Snura amesema, kupitia kwenye Ukurasa wake wa Instagram kuwa, hilo ni tukio kubwa sana kwake katika historia ya maisha yake.

”Nashukuru sana kuwa mwanamke wa kwanza kuvishwa kofia na Rais wetu Dkt John Magufuli. Msanii wa kike wa kwanza Rais kuvua kofia yake kunivalisha, hii ni kubwa sana kwangu. Ndani ya mkoa wa Tabora sitosahau historia hii, kwangu mimi ni baraka kubwa sana nimepewa leo.

“Rais Magufuli, kwa kuniheshimisha nakushukuru sana na Asnte sana, ama kwa hakika huyu ni rais mwenye upendo sana, na kupitia Chama Changu Cha Mapinduzi leo (jana), nimepata heshima hii kubwa kama mwanamke.. Asanteni sana viongozi wangu wote wa chama,” amesema Snura.

Hata hivyo Snura amesema, Mungu akitaka kukuheshimisha hakuna anaeweza kukudharaulisha, hivyo amemshukuru Mungu kujibu kile ambacho anakifanya ktik kazi y sanaa.

%%%%%%%%%%%%%%