January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Snoop: kuacha bangi ilikuwa kiki tu

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

MSANII wa muziki wa Hip pop nchini Marekani, Snoop Dogg amesema kitendo cha kutangaza kuwa ameacha uvutaji wa Bangi si cha kweli, bali ilikuwa kiki kwa ajili ya Ku-Promote Tangazo la Kampuni ya Majiko “Solo Stove”

Kampuni hiyo inatengenza majiko yanayowaka moto bila kutoa Moshi. Kwenye Majimbo ya Marekani na nchi zenye baridi kali majiko hayo hutumika katika kuotea moto.

Snoop, rapper na mdau anayejulikana katika uvutaji wa bangi, wiki iliyopita alisema kupitia kwenye mitandao ya kijamii kwamba “anaacha kuvuta bangi,” na kuwafanya mashabiki kuhoji kulikoni.

Katika tangazo hilo, Snoop Dogg, ambaye jina lake halisi ni Calvin Broadus, ameonekana anachoma marshmallows mbele ya shimo la moto la chuma cha chapa ya Solo Stove.

Rapa huyo, mwenye umri wa miaka 52, amekuza uvutaji wa bangi kwa muda mrefu kwenye kazi yake, huku akitumia picha za mmea huo kwenye jalada la albamu yake na video zake za muziki.