November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Smart Mwenyekiti mpya CCM

Na Daud Magesa, Timesmajira Online, Mwanza

MACHAEL Lushinje Masanja (Smart) amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza kwa kura 784 kati ya 1,111 na kuwashinda wagombea wenzake wanne waliopata kura 299 kwa pamoja huku kura 28 zikiharibika.

Uchaguzi huo umefanyika Desemba 4,2023 kuziba nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Sixbert Ruben aliyeteuliwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Masasi (DED) mkoani Mtwara.

Msimamizi wa uchaguzi huo Mjumbe wa NEC na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Said Mtanda akitangaza matokeo hayo amesema wagombea walikuwa ni Michael Lushinge Masanja (Smart),David Mayala Mulongo, Sabana Lushu Salinja, Elizabert Watson Nyingi na Dkt.Angelina William Samike.

Amesema wajumbe waliojiandikisha kupiga kura walikuwa 1,155 lakini waliopiga ni 1,111 kura 28 ziliharibika na kura halali zilikuwa 1,083 ambapo Michael Lushinge Masanja almaarufu Smart alipata kura 784 kati ya zilizopigwa.

Mtanda amesema Sabana Lushu Salinja alipata kura 250, David Mayala Mulongo 20, Dr.Angelina William Samike 15 na Elizabeth Watson Nyingi 7 hivyo akamtangaza Michael Lushinge Masanja au Smart kuwa Mwenyekiti mpya wa CCM Mkoa wa Mwanza kwa kura 784.

NayeSabana Salinja akizungumza baada ya matokeo amesema uchaguzi ulikuwa huu na haki na kwamba wajumbe wamewapigia kura wagombea wote na si ushindi wa Masanja au Smart bali wa wana Mwanza wote na kuahidi ushirikiano lea mwenyekiti2 mpya.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa kiti hicho,Smart ambaye alikuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Misungwi kabla ya uchaguzi huo amewapongeza wagombea wote na wajumbe kwa kura walizompa ambapo zimempa deni la ushirikiano.

“Tuna kazi ya kufanya baada ya uchaguzi nayao ni kushirikiana ili tuwe imara kuelekea auchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu 2025 pia ushirikiano unahitajika ili kutekeleza yanayokihusu Chama Cha Mapinduzi ili kuleta maendeleo ya wananchi,”amesema.

Awali Mwenyekiti wa muda Mjumbe wa NEC mkoani Mwanza, Jamal Abdul akifungua mkutano huo wa uchaguzi amesema wajumbe kuchagua kiongozi mzuri atakayetende haki kwa wanachama wote.

“Baada ya uchaguzi huu Mwenyekiti anayekuja Mwanza hatutaki kuwe na nyufa za makundi na mpasuko,tuleee chama hakuna mtu wa kuonewa,Mwanza ni dira ya siasa Kanda ya Ziwa na inatizamwa kwa jicho la tatu,kiongozi ni anayetenda haki hatutaki kiongozi wa kuonea wanachama,”amesema.