March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Skauti Rukwa waadhimisha siku ya Powell kwa kupanda miti

Na Israel Mwaisaka, Timesmajira Online-Rukwa

‎Skauti Mkoa Rukwa wameiazimisha siku kumbukizi ya kuzaliwa kwa mwanzilishi wa Skauti duniani  Sir Roberth Barden Powell,kwa kupanda miti na kufanya matendo ya huruma katika hospitali ya Wilaya ya Nkasi.

‎Akiongoza zoezi hilo Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya Nkasi ambaye pia Ofisa Uhamiaji wa Wilaya hiyo,Mrakibu Mwandamizi,Aloyce Fuko, amezema wazo hilo la uoandaji miti linaenda sambamba na matamanio ya Rais Dkt,Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha tunakabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kupanda miti.



‎Amesema kutokana na shughuli nyingi za kibinadamu miti mingi imekua ikikatwa na kuweka taifa katika mazingira hatarishi yanayotokana na uharibifu huo wa mazingira.Hivyo kitendo cha Skauti cha kuja na wazo hilo katika kumbukizi ya mwanzilishi wa Skauti duniani ni kulitendea haki taifa.

‎Awali Kamishna wa Skauti Mkoa Rukwa, Hassan Kikoloma,amesema licha ya zoezi hilo la kupanda miti pia watawatembelea wagonjwa wa hospitali ya wilaya Nkasi na kuwapatia zawadi mbalimbali ikiwemo sabuni na vitu vingine.

‎Amesema, mwanzilishi wa Skauti duniani aliwaongoza watu katika matendo ya huruma na kuonesha upendo na amani na matendo yake yamekua muongozo kwa Skauti kote duniani na ndiyo maana leo wanayafuata kwa kuwashika mkono wagonjwa.

‎Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya Nkasi,Dkt.Thomas Ndeule,amesema eneo la hospitali hiyo ni jipya hivyo miti mingi ilikatwa wakati wa ujenzi hivyo upanddaji wa miti uliofanywa na Skauti hospialini hapo ni jambo jema.

Amesema kuwa kama viongozi wa hospitali hiyo watahakikisha miti hiyo inalindwa na kukua na kuwaomba Skauti wakati mwingine waendelee kuikumbuka hospitali hiyo katika eneo hilo la upandaji miti.