Na Judith Ferdinand, TimesMajira Online Mwanza
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Reuben Sixbert,ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti CCM Mkoa wa Mwanza,baada ya kuwashinda wapinzani wake kwa kura 879.
Akizungumza mara baada ya zoezi la kupiga kura kukamilika katika mkutano mkuu wa CCM mkoani Mwanza uliofanyika Novemba 21, 2022 uwanja wa CCM Kirumba, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Taifa ambaye pia ni msimamizi wa uchaguzi wa CCM mkoa wa Mwanza Gilbert Kalima alimtangaza Reuben Sixbert kuwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza.
Ambapo katika nafasi hiyo ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa ilikuwa na wagombea watatu waliojitokeza kuwania nafasi hiyo,ambao ni Ruben Sixbert,Nyirizu Makongoro na Nyanda Elias.
Kalima, ameeleza kuwa katika uchaguzi huo jumla ya wapiga kura walikuwa 1127,zilizoharibika ni 2 hivyo kura halali ni 1125, huku Ruben Sixbert akishika nafasi ya kwanza kwa kupata kura 879,akifuatiwa na Nyirizu Makongoro aliyepata kura 239 huku Nyanda Elias akiambulia kura 7.
Ameeleza kuwa zoezi hilo la uchaguzi lilikuwa gumu sana huku akitoa pongezi kwa wapiga kura sanjari na kuwataka wagombea wote ambao kura hazijatosha wajipange tena katika uchaguzi ujao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Reuben Sixbert, akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi aliwaomba Wenyeviti wa CCM Wilaya na Kata waungane kwa pamoja katika kusaidia utekelezaji wa ilani ya chama pamoja na kuwaunganisha wana CCM.
Aidha ametumia fursa hiyo kuwahimiza wanaCCM kutopambana wao kwa wao bali wapambane na vyama vya upinzani, hivyo wajiandae vyema kwa ajili ya chaguzi za Serikali ya Mitaa mwaka 2024 na Mkuu mwaka 2025.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza aliemaliza muda wake Antony Diallo,amewahimiza viongozi hao wapya kuendeleza juhudi za ujenzi wa ofisi mpya za CCM katika majimbo ya Sumve na Buchosa.
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua