March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Siriwa:Vyama vya Siasa hubirini amani kuepuka vurugu

Na Penina Malundo,Timesmajira

 KATIBU Mkuu wa Taasisi  ya Tanzania Jumuishi (TAJU),Innocent Siriwa  amevikumbusha vyama vya siasa nchini kuona umuhimu na wajibu wakulinda na  kuhubiri amani ili kuepuka vurugu kama zilizotokea katika uchaguzi wa Oktoba 29 mwaka huu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana wakati akiongea na waandishi wa habari  alisema ni wakati wa wanasiasa kuhubiri amani na kuhakikisha kila mmoja wetu anailinda na kuitunza.

“TAJU  inavikumbusha vyama vya siasa vyote na viongozi wa dini  kutumia nafasi zao ili kulinda na kuhubiri amani ya nchi yetu ili nchi iendelee kuwa na utulivu,”amesema Siriwa.

Amesema taasisi hiyo pia inawataka watanzania kuacha kuiga mambo ya nje ambayo hayana tija na yanaliingiza Taifa katika vurugu.

“Watanzania waache  watanzania kutumia mitandao vibaya na kufanya mambo maovu badala yake uchagua mema na kuacha mabaya mfano tabia za ushoga,maandamano ya vurugu kwakuwa yapo maandamano ya amani yenye agenda  yenye mabango yanayojieleza na utaratibu unaokubali kijamii na yenye muda wakuweka shindikizo ili kutekeleza suala hilo”amesema Siriwa.

Akizungumzia kuhusu vurugu za Oktoba 29 ametoa pole kwa wananchi waliopatwa na kadhia hiyo na kusisitiza kuendelea kuimarisha amani.

:Inawezekana wapo waliopata ulemavu na kuingia kwenye kundi letu bila hiyari tunatoa pole kwa watoto wote wenye ulemavu,Taju inawakumbusha watanzania wakubwa na wadogo wake kwa waume wakati wote ni muhimu wakulinda nchi yetu,”amesema Siriwa.