Na Penina Malundo,Timesmajira
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene amesema Tanzania na Afrika kwa ujumla inahitaji viongozi wa kimageuzi katika kuhamasisha juhudi za pamoja katika kutimiza malengo yapamoja.
Pia kusaidia kuhamasisha uvumbuzi, kuongoza mabadiliko katika nyanjaza kiuchumi na kijamii, pamoja na kuandaa na kutekeleza Sera zinazokuzamaendeleo jumuishi na endelevu ya Bara la Afrika.
Simbachawene ameyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wa mahafali ya nane ya Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute) yaliyofanyika ukumbi wa Mlimani City huku zaidi ya wahitimu 200 wakifuzu mafunzo yanayotolewa na taasisi hiyo.
Amesema viongozi wa kimageuzi wana sifa ya kuwa na maono ya kuleta mabadiliko ambayo yana uwezo wa kufanya maamuzi ya kimkakati,kuibua fursa mpya za Maendeleo, kuwasilisha na kushawishi mipango ya muda mfupi na mrefu ya kukuza uchumi na kuboresha hali ya maisha ya jamii zao.
Amesema mafunzo waliyoyapata yatawasaidia kuwa na maono,kusimamia utekelezaji wa mipango ya pamoja na kupima na kufanyamapitio ya matokeo ya utekelezaji wake.
“Ni matumaini yangumtakuwa na uwezo mkubwa wa kutambua fursa na kuchangia katikakuweka mazingira mazuri ya kiuongozi yatakayochochea kuleta maendeleoendelevu nchini mwetu.

“wito kwa viongozi kubuni mbinu madhubuti za kuratibu utekelezaji wa miradi ili kuhakikisha matumizi bora ya rasilimali fedha na watu katika kuleta matokeo chanya na yenye tija nchini,”Amesema.
Amesema serikali inafanya uwekezaji mkubwa wa kifedha kwenye miradi nchini ili kuchochea maendeleo ya taifa na kuboresha maisha ya wananchi wetu hivyo ni muhimu viongozi kubuni mbinu madhubuti za kuratibu utekelezaji wa miradi hiyo.

Aidha amesisitiza kuwa suala la uratibu wa miradi ya maendeleo umekuwa na changamoto nyingi zinazoathiri ufanisi hivyo amewaomba viongozi huko waendako wakasaidie kutafuta namna bora zaidi za kuratibu utekelezaji wa miradi katika njia itakayosaidia matumizi ya rasimali fedha na watu ili ilete matokeo makubwa na chanya.
“Kama mnavyofahamu, Serikali inawekeza pesa nyingi sana katika miradi hiyo ili kuleta maendeleo na kuimarisha ustawi wa wananchi. Jambo hili litawezekana kama tutaimarisha mawasiliano na mahusiano na wadau wetu wa masuala ya maendeleo ndani na nje ya mipaka ya nchi yetu,” amesema

Aidha amesema katika mafunzo ya Uongozi wahitimu wafundishwa juu ya umuhimu wa ubunifu na uvumbuzi, uthubutu, namna ya kuongoza watu na kusimamia rasilimali, kushirikiana, kuheshimiana na kutenda haki, masuala muhimu ya maadili na utawala bora pamoja na athari za rushwa katika kutekeleza majukumu yao kama watumishi.
“Yote haya yatoshe kusema sasa tunataka kuona utumishi bora wenye misingi imara na thabiti yakiuongozi. Hatutegemei kuona mnaowaongoza au nyie wenyewe mkijihusisha na masuala ya rushwa, ubadhilifu, uzembe, uvivu na vitendo vya unyanyasaji ndani na nje ya kazi.
“Tunatarajia ninyi muwe chachu na mstari wa mbele wa mabadiliko kwa sababu mmepata fursa ya kupata mafunzo haya muhimu. Nendeni mkatende haki, mkafanye maamuzi sahihi yatakayo saidia kuondoa kero za wananchi na kuboresha utoaji huduma,” amesema Simbachawene

Naye Mke wa Rais wa Finland, Suzanne Innes-Stubb, amewashauri viongozi nchini kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, utawala bora na kufanya maamuzi mbalimbali kwa kuzingatia ukweli.Innes-Stubb amesema kuwa kuna madhara ya taarifa potofu na upotoshaji kwa sasa kutokana na maendeleo ya teknolojia ni makubwa, hivyo viongozi wanapaswa kufanya maamuzi kwa kuzingatia ukweli na si kwa dhana au hisia.

Naye Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Zena Ahmed Said, amewahimiza viongozi kutumia ujuzi walioupata kuwahamasisha wengine na kuchangia maendeleo yenye maana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Uongozi, Kadari Singo,amesema zaidi ya viongozi 200 wamehitimu katika programu hizo tatu, ambazo zimehudhuriwa na viongozi kutoka bara zima na kutoka sekta mbalimbali kama serikali, biashara, elimu ya juu na asasi za kiraia.
More Stories
Mhandisi Samamba ahimiza uaminifu kwa watoa huduma migodini
Mwanasheria Mkuu wa Serikali awataka wananchi kujitokeza kujiandikisha daftari la wapiga kura
Dkt.Mpango azindua shule ya sekondari itakayojengwa na CRDB Dar