*Atembelea Banda la Wizara ya Nishati na Taasisi zake Wiki ya Utumishi wa Umma
Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene ameiasa Wizara ya Nishati kuendelea kuweka mazingira wezeshi yatakayowezesha uwekezaji zaidi wa vituo vya mafuta vijijini.
Simbachaene ameyasema hayo leo Jini 17, 2025, jijini Dodoma, alipotembelea Banda la Wizara ya Nishati katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Chinangali ambayo leo yamefunguliwa rasmi

“Wafanyabiashara wengi wanataka kuwekeza kwenye vituo vya Mafuta vijijini kwakuwa bado kuna uhaba wa vituo, hivyo angalieni masharti yanayowekwa kwenye uwekezaji yasiwe kikwazo kwenye huduma hii muhimu.” Amesema Simbachawene
Pia, Simbachawene ameishauri Wizara kuongeza kasi ya upatikanaji wa Nishati Safi ya Kupikia Vijijini pamoja na kuhamasisha uwekezaji kwenye Nishati Safi ya Kupikia.
Vilevile, ameipongeza Wizara ya Nishati na Taasisi zake kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuendelea kutoa huduma za Nishati kwa wananchi.




More Stories
Wanawake jumuia ya kikristo Tanzania CCT wafundana kuelekea siku ya Wanawake Duniani
Dkt.Tulia,Mwalunenge waungana kutatua changamoto ya barabara
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi