Na Mwandishi Wetu
MABINGWA wa msimu uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) ambao wataiwakilisha nchi katika mashindano ya Klabu Bingwa Afrika, Simba wamepangwa kukutana na timu ya Plateau United FC kutoka Nchini Nigeria katika raundi ya awali ya mashindano ya hayo.
Katika michuano hiyo Simba itaanzia ugenini katika mchezo utakaochezwa kati ya Novemba 27 na 29 huku mchezo wa marudiano ukichezwa kati ya Desemba 4 na 6.
Mshindi wa jumla wa mchezo huo, atakutana na mshindi wa jumla katika mchezo kati ya Costa do Sol ya Msumbiji au FC Platinum ya Zimbabwe.
Wapinzani wa Simba walipata nafasi ya kushiriki mashindano hayo baada ya kuongoza katika msimamo wa Ligi Kuu Nchini humo wakati Ligi ya nchini humo inafutwa kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Covid- 19.
Katika mechi 25 ambao walikuwa wamecheza, Plateau United walikuwa wakiongoza kwa kuwa na pointi 49 baada ya kushinda mechi 14, sare saba na kupoteza mechi nne ambazo walifungwa na Heartlang, Abia Worrious, Katsina United na Sunshine Stars.
Timu hiyo pia ilikuwa ikiongoza kwa magoli ya kufunga ikifanikiwa kufunga goli 36 lakini pia imeruhusu goli chache 15 ukilinganisha na timu nyingine katika msimamo wa Ligi hiyo.
Pia walikuwa wamewazidi pointi 13 Enyimba ambao walikuwa wakishika nafasi ya pili katika msimamo huo wa ligi wakiwa na pointi 36 huku wakiwa wamecheza mechi 20.
Katika mashindano hayo Simba inatakiwa kuhakikiwa wanajipanga vema ili kupata ushindi ugenini na nyumbani ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kusonga mbele uukilinganisha na msimu uliopita ambapo walitolewa katika atua ya awali ya timu ya UD Songo kutoka Msumbiji.
Mbali na Simba, wawakilishi wengine wa Tanzania timu ya Mapunduzi kutoka Zanzibar imepangwa kukutana na Sfaxien kutoka nchini Tunisia.
Katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika, timu ya Namungo FC itaanzia nyumbani dhidi ya wapinzani wao timu ya Al Rabita kutoka Sudan Kusini.
Timu ya Gormahia itakutana na APR na mshindi wa mchezo huo atakutana na msindi wa mchezo kati ya CR Belouizdada na AL Nasri.
Katika ratiba hiyo pia FC Nouadhibou watamenyana na Asante Kontoko, Buffels atacheza dhidi ya MC Algers, Enyimba atamenyana na Rahimo FC, AS Otoho amekutana na Al Merreikh wakati timu ya Costa do Sol atacheza dhidi ya FC Platinum.
Washindi katika hatua hii watakutana na timu ambazo hazitashiriki katika raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambazo ni Al Ahly na Zamalek za Misri, AS Vita na TP Mazembe za Congo, Esperance ya Tunisia, Horoya ya Guinea, Mamelond Sundowns ya Afrika Kusini, Raja Casablanca na Wydad Casablanca za Morocco.
More Stories
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes
Rais Samia: Yanga endeleeni kuipeperusha bendera ya Tanzania