December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Simba, Yanga zaingiza milioni 269

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, DSM

MCHEZO wa nusu fainali wa Kombe la Shirikisho la Azam (Azam Sports Federation Cup) kati ya watani wa Jadi Simba na Yangaumeingiza Sh milioni 269,100,000.

Katika mchezo huo ambao ulimalizika kwa Simba kutinga fainali baada ya kuwachapa Yanga goli 4-1 tiketi ziliouzwa kwa upande wa VIP A ni 93 ambazo zinengiza Sh. 2,790,000.

Kwa upande wa VIP B jumla ya tiketi zilizouzwa ni 1,520 ambazo zimeingiza Sh milioni 38,000,000, VIP C imeingiza Sh. milioni 29,080,000 baada kuuzwa kwa tiketi 1,454 huku tiketi ziliouzwa kwa mzunguko ni 19,623 n kuingiza milioni 199,230,000.