January 16, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Simba, Yanga kupangiwa tarehe mpya, viingilio kurejeshwa

Baada ya jana Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, Kassim Majaliwa kuingilia kati sakata la kuahirishwa kwa mechi namba 208 ya Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) kati ya Watani wa Jadi Simba na Yanga iliyotakiwa kuchezwa Mei 8 katika uwanja wa Benjamin Mkapa na kuiagiza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kutoa taarifa za kina juu ya sakata hilo, hatimae Wizara imeweka wazi taarifa rasmi baada ya kikao kilichowakutanisha viongozi mbalimbali ikiwemo wa Shirikisho la Soka nchini (TFF).