January 24, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Picha kwa hisani ya SSC Tanzania.

Simba, Yanga kucheza nusu fainali FA Cup

Na Hamis Miraji, TimesMajira Online

MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba, leo wamefanikiwa kutinga nusu fainali ya Kombe la Shirikisho (FA), baada ya kuifunga Azam FC goli 2-0 katika mchezo wa nusu fainali uliofanyika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Mchezo huo ulikuwa wa vuta nikuvute huku Simba ikionekana kuutawala mchezo kwa asilimia kubwa.

Simba walijipatia goli lao la kwanza dakika ya 39 kupitia kwa mshambuliaji wake John Bocco, baada ya kuunganisha kwa kichwa klosi ya Francis Kahata.

Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko lakini Simba walifanikiwa kwa kiliandama kama nyuki lango la Azam FC.

Hata hivyo dakika ya 56 Simba waliandika goli lai pili kupitia kwa kiungo wake Cretus Chama baada ya kuunganisha pasi safi ya Shomari Kapombe.

Kwa matokeo hayo Simba watacheza na Yanga nusu fainali huku Sahare United watacheza na Namungo.