Na Mwandishi Wetu
KOCHA Mkuu wa Simba, Franco Pablo Martin amesema kikosi cha timu yake kimedhamiria kumaliza kinara wa ‘Kundi D’, katika michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika hatua ya makundi.
Simba inaongoza msimamo wa ‘Kundi D’, baada ya kuifunga RS Berakane bao 1-0 mwishoni mwa wiki, mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, na kufikisha alama saba.
Akizungumzia hilo, Kocha Pablo amesema hatua ya kuamaliza kinara wa Kundi D ni heshima kwa klabu ya Simba Barani Afrika, pia timu yake itapata nafasi ya kucheza Robo Fainali ikianzia ugenini na kumalizia nyumbani.
“Malengo yetu kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho msimu huu ni kuhakikisha tunacheza angalau nusu fainali, na katika kufanikisha hilo ni wazi tunapaswa kufanya kazi kubwa katika michezo yetu ya mwisho ili kuhakikisha tunapata matokeo, yatakayotuvusha na kutinga hatua ya Robo Fainali.”
“Tunataka kumaliza kama vinara wa kundi hili, ambapo hiyo itatusaidia kwa kiasi kikubwa kuwa na bahati ya kuanzia ugenini na kumalizia hapa nyumbani.” amesema Kocha huyo kutoka nchini Hispania.
Simba SC itacheza dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast katika mchezo wa Mzunguuko watano wa ‘Kundi D’ Jumapili (Machi 20) nchini Benin.
More Stories
Kasulu FC mabingwa mashindano Khimji 2025
Fainali Khimji cup kufanyika Februari 7,2025
Naibu Waziri wa Fedha abariki ujio mpya wa Bahati Nasibu