Na Ashura Jumapili,TimesMajira online Kagera
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Daniel Sillo ameitaka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Kagera kushirikiana ili kuboresha utendaji kazi.
Ametoa agizo hilo ikiwa ni maelekezo ya Katibu Mkuu wa huyo akiwa wilayani Ngara mkoani Kagera na kuelezwa na wananchi kuwa bado wanachangamoto ya upatikanaji wa Vitambulisho vya Taifa.
Kauli hiyo ameitoa wilayani Muleba mkoani Kagera katika mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ambapo amewataka kushirikiana na kufanya kazi kwa weledi na uadilifu ili kuwezesha upatikanaji wa vitambulisho vya Taifa kwa wakati.
” Uhamiaji na NIDA shirikianeni katika suala zima la utambuzi na usajili wa wananchi ili kuharakisha upatikanaji wake kwa Wananchi wenye sifa.Sitegemei kuona jambo lolote kukwamisha vitambulisho hivyo bila sababu za msingi,”amesema Sillo.
Hata hivyo amemuelekeza Ofisa Usajili wa NIDA kuwa hakikishe vitambulisho 78,766 ambavyo bado havichukuliwa viwafikie walengwa huku akitoa wito kwa wananchi kwenda kuchukua vitambulisho hivyo katika Wilaya, Kata na Vijiji vilivyopo karibu nao.
More Stories
Waziri Mkuu: Tumieni matokeo ya tafiti za kisayansi katika utekelezaji wa mipango ya kitaifa
Zaidi ya wananchi 32,000 Vijiji vya Wilaya za Morogoro na Mvomero kuanza kupata mawasiliano
Wafanyabiashara waomba elimu ya namna watakavyorejea soko kuu