Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
MBUNGE wa Jimbo la Ukonga, ambaye ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jery Silaa, amewataka wananchi wa jimbo la Ukonga mwaka 2025 kumpigia kura Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ili aweze kuibuka kwa kishindo kwenye uchaguzi mkuu wa Rais wabunge na madiwani 2025 .
Mbunge Jery Silaa alitoa agizo hilo katika mkutano wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2023 /2024 iliyowasilishwa na Diwani wa Kata ya Msongola AZIZI MWALILE.
“Wananchi wangu wa jimbo la Ukonga Namshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kutoa Waziri kwa mara ya kwanza katika Jimbo la Ukonga aijawai kutokea toka nchi yetu ipate Uhuru mwaka 1961 Namshukuru Rais ameona Jery Silaa ninatosha kuwa Waziri wa ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi nawaomba Wananchi wangu wa Jimbo la Ukonga Mwaka 2025 kura za Rais zote ziende kwa Dkt.Samia ili aweze kupeperusha Bendera ya CCM “alisema Silaa.
Mbunge Jery alisema wakati anaingia madarakani
awali barabara ya Lami ilikuwa inaishia Pugu kwa sasa Serikali imeweka barabara ya lami Jimbo la Ukonga Chanika yote kwa sasa Barabara ya Lami inatokea Mbande Mbagala,Temeke kuelekea Chanika yote hayo ni matunda ya Serikali hivyo wananchi hawana budi kumpigia kura Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Aidha alisema kwa sasa mkakati wa Serikali hivi karibuni ujenzi wa barabara ya Lami utaanza Banana ,Kitunda ,kuelekea Kivule pamoja na Taa za kisasa hivyo wananchi wavute subira kusubiria matunda ya Serikali ya awamu ya sita ZABUNI ameshatangazwa wa Barabara za Kisasa Jimbo la Ukonga na wananchi wataenda shugudia siku ya kukabidhiwa tenda .
Akizungumzia sekta ya maji alisema maji yapo CHANIKA na ZINGIZIWA ambapo MGEULE wanafunga Tanki kwa ajili ya kusambaza maji Msongola yote
More Stories
AZAKI yawasilisha mapendekezo yao kwa Serikali katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050
CP.Wakilyamba :Uvamizi maeneo ya hifadhi ya taifa katavi haukubaliki
Watu wawili wanaodhaniwa majambazi wapigwa risasi na Polisi