November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Silaa atoa siku saba kutatua migogoro ya ardhi Dar

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jery Silaa, ametoa siku saba kwa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi kuja na Mpango Mkakati wa kutatua na kumaliza Urasimishaji katika mkoa Dar es Salaam.

Waziri Silaa, ametoa agizo hilo leo katika kikao cha Halmashauri ya chama cha Mapunduzi CCM Mkoa Dar es Salaam kilichowashirisha Wakuu wa Wilaya wote, Watendaji wa Wizara ya Ardhi na Mameya wa mkoa huo.

“Nakuagiza Katibu Mkuu wa wa wizara yangu kero ya urasimishaji imekuwa kubwa katika mkoa huu nakupa siku saba kuja na mpango kazi kwa ajili ya kuyafanyia kazi malalamiko kuhusiana na kampuni za Urasimishaji zilizofanya vibaya ufumbuzi upatikane na kuakikisha zinachukuliwa hatua “alisema Jerry.

Waziri Jery Silaa alisema katika mkoa Dar es Salaam ni mara ya kwanza kuongea na Halmashauri kuu ya Mkoa huo anamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa imani kubwa kazi hiyo anaifanya vizuri na kuomba ridhaa mwaka 2025.

Alisema wakati wote atafanya kazi hiyo kwa uadilifu mkubwa ili chama cha Mapinduzi CCM kiweze kusonga mbele kwani kitendo cha kuitwa na ccm mkoa wanatambua mchango wake wa utekelezaji wa Ilani.

“Nimekuja na Watendaji wangu wote wa wizara ya ardhi Ilani ya CCM ilitoa ahadi kwamba tutafanya kazi ndani ya miaka mitano kutatua migogoro ya ardhi ndani ya miaka mitano tutatoa hati milioni 2.5 wananchi waweze kumiliki ardhi” alisema.

Alisema Mkoa Dar es Salaam mda mrefu aujapimwa na kupangwa kutokana na changamoto ya Watumishi na vifaa sababu Serikali aina vifaa vya kutosha ilitoa kazi hiyo kwa kampuni za urasimishaji wasimamie kurasimisha maeneo yote.

Alisema mikakati ya wizara hiyo itatoa urasimishaji karibu na wananchi na kuwa na Kamishina kila wilaya itakuwa na kamishina wa Mkoa wa ardhi dhumuni na malengo ya Serikali kusogeza huduma kwa wananchi.

Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM mkoa Dar es Salaam Abbas Mtemvu , alimpongeza Waziri wa ardhi Jery Silaa ni msikivu anashirikiana na chama na Serikali vizuri amekuja kusikiliza migogoro ya ardhi katika mkoa huo.

Mwenyekiti Abas Mtemvu alitoa agizo migogoro yote ya ardhi inayohusiana na chama ameagiza waorodheshe na kumpelekea Katibu wa mkoa wa ccm ili aweze kupeleka wizarani Serikali ipatie ufumbuzi wake mara moja .

Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonnah Ladslaus Kamoli alisema katika jimbo la segerea urasimishaji ni changamoto kata zote ikiwemo Kisukuru hivyo ameomba Serikali kwa kushirikiana na Wizara kutatua changamoto hizo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango Miji Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam ambaye ni Diwani wa kata ya Kivule Nyasika Getama, alisema urasimishaji katika jiji hilo ni janga mitaa yote 159 hasa Kata ya Kivule Zoezi limekwama .

Mwenyekiti Nyasika Getama alisema pia migogoro wa wilaya ya Kisarawe na Ilala umepatiwa ufumbuzi bado kuweka Bikoni,kata zingiziwa,Chanika,Buyuni,Pugu na Pugu Station. Mpaka wilaya Temeke na Ilala ,Kitunda,mtaa wa Kipera,Kivule (UVIKIUTA)na mkuranga na Ilala Msongola wanaomba utatuzi wake ili mwaka 2024 chama cha Mapunduzi kiweze kuingia katika mchakato wa uchaguzi wa kushika dola bila changamoto.