Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma
SERIKALI kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara, imesema ndani ya siku 100 za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan madarakani katika kipindi chake cha pili cha Urais, Wizara hiyo imefanikiwa kutoa mikopo yenye thamani ya Tsh. milioni 821.7 ambayo imezalisha Viwanda vidogo na kuleta ajira za moja kwa moja 546 ikiwemo ajira 436 za Vijana.
Hayo yamesemwa jijini hapa hayo leo Januari 24,2026 na Waziri wa Viwanda na Biashara Judith Kapinga wakati akizubgumza na Waandishi wa Habari kuhusu mafanikio ya utekelezaji wa ahadi za Rais Samia katika siku 100 za kwanza katika uongozi wake wa kipindi cha pili cha miaka mitano ya awamu ya sita.

Amesema kuwa katika siku 100 Rais Samia aliahidi kutenga fedha kwa ajili ya upatikanaji wa mitaji kwa Wafanyabiashara wadogo na wa kati na kuwezesha kampuni changa.
“Kwa upande wetu Wizara ya Viwanda na Biashara tumeunga mkono utekelezaji wa ahadi hii kuanzia Novemba 2025 hadi leo Januari 2026, kupitia SIDO tumetoa mikopo yenye thamani ya Tsh. milioni 821. 7 kupitia mfuko wa uendelezaji wa Wajasiriamali kwa Vijana katika Mikoa 19, mikopo ambayo imezalisha viwanda vidogo na kuleta ajira za moja kwa moja 546 katika sekta za viwanda, ufugaji, kilimo, biashara na huduma na katika ajira hizo 546, ajira 436 ni kwa Vijana na ni ajira za moja kwa moja na hata hivyo zimechangia ajira za moja kwa moja zaidi ya 1000”amesema.
Aidha Waziri Kapinga amesema kuwa zaidi ya vijana 1,200 wamepatiwa mafunzo ya ujasiriamali, huku mamia yao wakiunganishwa na programu za uatamizi wa biashara kwa lengo la kuwawezesha kukua kibiashara.

Vilevile amesema katika siku 100 hizo Wizara kupitia BRELA imeweka msukuko mkubwa katika urasimishaji wa biashara na ulinzi wa ubunifu ambapo Kampuni 4,233 zimesajiliwa, kati ya hizo 2,915 ni za vijana.
Pia majina ya biashara 7,498 yamesajiliwa, ambapo 4,742 kati yake ni ya vijana,alama za Biashara na Huduma 881 zimesajiliwa,leseni za Viwanda 141 zimetolewa, kati ya viwanda hivyo 129 ni vya vijana na Leseni za Biashara Kundi “A” 4,907 zimetolewa.

More Stories
Dkt.Tulia,Mwalunenge waungana kutatua changamoto ya barabara
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi
Kihongosi:Uhai wa chama mashina