December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

SIDO Arusha lawafikia wajasiriamali 509

Na Queen Lema, TimesMajira Online, Arusha

Shirika la kuhudumia viwanda vidogo vidogo mkoa wa Arusha(SIDO)limefanikiwa kuwafikia wajasiriamli 509 wa mkoa wa Arusha huku lengo likiwa Ni kuwafikia wajasiriamli 800 kwa mwaka

Hayo yameelezwa na Afisa biashara Uendelezaji kutoka SIDO Bi Bahati Mkopi wakati akiongea na vyombo vya habari mapema Jana kuhusiana na Mafunzo ambayo Shirika Hilo linatoa kwa wajasiriamli mkoa wa Arusha.

Bi Bahati alisema kuwa wajasiriamli ambao wamezalishwa pia wameweza kuibua mafanikio makubwa Sana na kuanzisha viwanda

Alidai kuwa wajasiriamli hao 509 ambao wamepita Sido wameweza kuwa chachu ya maendeleo Kwa kuwa mbali na kuanzisha viwanda pia wameibua ajira nyingi sana tofauti na hapo awali ambapo viwanda havikuwepo

Aliongeza kuwa hata idadi ya viwanda kwa mkoa wa Arusha nayo imeongezeka na mpaka sasa kuna viwanda zaidi ya 1250 ambavyo vinazalisha bidhaa mbalimbali

“Tunajivunia Sana uwepo wa viwanda na wajasirimali nao wameweza kukua lakini haitoshi kusema Tu tumetosheka bado tunataka kuzalisha viwanda vingi zaidi na zaidi na sasa tunataka kuwafikia walio wengi na ndani ya wiki Hii sasa tutakuwa na Mafunzo ambayo yanalenga kuongea ubora wa bidhaa”aliongeza Bahati

Akiongelea Mafunzo ambayo watatoa kwa wajasiriamli Kwa wiki moja alisema kuwa nayo yanalenga kuipa thamani bidhaa ambazo zinapatikana kwenye jamii kwa Uraisi.

“Tutawafundisha mambo mbalimbali kama vile kuongeza thamani ya mazao ya kilimo,kuboresha kiwanda,pamoja na ubora wa kiwanda Kwa kuwa lengo letu Sisi ni kuanzisha biashara na viwanda ambavyo vina ubora wa kutosha”aliongeza

Alihitimisha kwa kusema kuwa ni wakati WA wajasiriamli Kwa mkoa wa Arusha kuhakikisha kuwa wanapata Mafunzo kutoka SIDO ambayo yataweza kuwafanya kufikia viwango vya kimataifa.