Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Ilala Said Sidde amewataka wana ccm Kata ya Mnyamani kujiandikisha katika Daftari la maboresho ya wapika kura ili waweze kupata haki ya kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka huu.
Mwenyekiti Sidde alisema hayo katika mkutano mkuu wa ccm tawi la Mnyamani ulioandaliwa na uongozi wa chama cha Mapinduzi wa tawi hilo.
“Tunaelekea katika uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka huu kila mmoja anayo haki ya kupiga kura mjitokeze kwa wingi katika kujiandikisha ili muweze kupiga kura chama chetu kishinde kwa kishindo” alisema Sidde.
Mwenyekiti Sidde alisema kila mwana ccm anayo haki ya kupiga kura uchaguzi ukifika hivyo akajiandikishe eneo Lake aweze kupata haki ya msingi ya kupiga kura.
Akizungumza katika mkutano mkuu maalum wa CCM Tawi la Mnyamani aliwapongeza uongozi wa CCM Kata ya Mnyamani kwa umoja wao ambapo aliwataka Mnyamani wasigawanywe kwa dini wala kabila badala yake aliwataka wajenge mshikamano kuwa wamoja katika kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa Rais wabunge na madiwani mwaka 2025.
Wakati huo huo aliwataka Mnyamani kuongeza usafi katika maeneo yao ili wajikinge na magonjwa ya mlipuko wakati huu wa mvua za masika wakikishe maeneo yao yanakuwa safi kila mmoja na kula vyakula vya moto.
Aliwagiza washirikiane na Serikali katika suala la utunzaji Mazingira yao na kufuata taratibu za usafi .
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mnyamani Mbaraka Mwinyivua aliwapongeza uongozi wa tawi la ccm Mnyamani kwa kuongeza Wanachama katika hilo wameongeza mtaji wa kutosha katika kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa Rais wabunge na madiwani mwaka 2025.
Mwenyekiti Mbaraka aliwataka wadumishe umoja wao ndio ushindi wao huku akiwataka washirikiane katika kufanya kazi za chama cha Mapinduzi kila wakati na kuitisha vikao .
Aliwataka wasimamie dhamana yao katika chama na kukitetea chama ikiwemo kusimamia Serikali na chama katika utekelezaji wa Ilani ya CCM.
Alitumia fursa hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan na Mbunge wa Jimbo la segerea Bonnah Ladslaus Kamoli kuleta miradi mikubwa ya kuboresha miundombinu ya Barabara ambayo inatarajia kuanza hivi karibuni ambapo kwa sasa Mnyamani wanajivunia maendeleo makubwa ukiwemo kujengewa shule ya kisasa na Serikali pamoja na Ofisi ya Afisa Mtendaji wa kata.
Mwenyekiti wa ccm tawi Mnyamani SADIKI MGAYA alisema dhumuni la mkutano huo kupokea wanachama wapya ambapo leo wamepokea wanachama 15 kutoka chama cha wananchi CUF ,ambapo CCM Mnyamani inaelekea katika mkutano wa Hadhara inatarajia kupokea wanachama wapya zaidi ya 70 na mikakati ya ccm Mnyamani kushika dola.
More Stories
Mwabukusi akemea wanasiasa wanaotoa kauli za kibaguzi kuelekea uchaguzi mkuu
TAA yatakiwa kulipia mirabaha inayohusiana na matumizi ya muziki katika viwanja vya ndege nchini
Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini yafanya ziara ya kujifunza uongezaji thamani wa madini nchini Zambia