Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala
SHULE ya Sekondari Uhuru Mchanganyiko wajivunia Mafanikio kitaaluma katika matokeo ya kidato cha pili na kidato cha nne kila mwaka wanafaulisha kwa kiwango cha juu.
Akizungumza katika mahafali ya 12 ya kidato cha nne Shuleni hapo Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Uhuru Mchanganyiko Abeid Kamugisha amesema shule hiyo ilianza mwaka 2007 ikiiwa na walimu nane na Wanafunzi 160 kwa Sasa mwaka 2022 shule ina Walimu 38 kati yao wanaume 14na wanawake 24 na wafanyakazi wanne .
“Kitaaluma shule inafanya vizuri kila Mwaka Mwaka Jana matokeo ya kidato cha nne yaliotangazwa na NECTA ilifanikiwa kufaulisha kwa asilimia 77 na matokeo ya mtihani wa mock tumefaulisha kwa asilimia 80 Mwaka huu 2022 watoto wetu watafaulu kwa kiwango Cha juu tumewandaa kwa Mazingira mazuri ” amesema Kamugisha.
Aidha amesema pia Wanafunzi wa Kidato cha pili wa shule hiyo Uhuru Mchanganyiko ambao wanatarajia kufanya mtihani wa NECTA Novemba 2022 takwimu za NECTA 2021 ufaulu ulikuwa asilimia 91 hivyo Vijana wetu wa Mwaka huu watafanya vizuri zaidi .
Mkuu wa shule amewataka Wanafunzi wanaomaliza kujiendeleza Kielimu mpaka chuo kikuu aliwataka wajilinde wasijitumbukize Katika vitendo viovu Vya utumiaji wa madawa ya kulevya.
“Nawaomba vijana wetu msome kwa bidii mzingatie masomo yenu Elimu aina mwisho nawaomba mzingatie masomo muweze kufika chuo kikuu ” amesema Kamugisha.
Kwa upande wa risala ya wahitimu wa kidato Cha nne iliyosomwa na Zuhura Maulid alisema shule ya Sekondari uhuru Mchanganyiko ina mchepuo wa Sayansi ,Sanaa na Biashara Zuhura alisema jumla ya wahitimu mwaka huu 2022 392 kati ya yao wavulana 196 na Wasichana 196 Zuhuru alitoa ushauri Kwa Serikali wanaomba kuongezewa Walimu wa Sayansi na chumba cha kompyuta kwa ajili ya Wanafunzi kusoma Somo la TEHAMA .
Aidha ametoa wosia kwa Wanafunzi wanaobaki wawe na maadili mema wawatii Walimu wawe na nidhamu wasome kwa bidii waweze kufikia malemgo yao.
Mgeni rasmi Diwani Fatuma Abubakari aliyemwakilisha Meya wa Halmashauri ya Jiji Omary Kumbilamoto amewaasa Wahitimu wa shule hiyo kuzingatia nidhamu wawapo shuleni Ili waweze kusonga mbele mpaka chuo kikuu .
Mwakilishi wa Meya Diwani Fatuma Abubakari alisema atafatilia Halmashauri mikakati ya ujenzi wa Shule ya gholofa Ili uweze kuanza mara moja .
Amesema pia atatatua changamoto za shule hiyo zikiwemo upungufu wa Walimu wa masomo ya sayansi .
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa