January 12, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Shule ya msingi Yongwe kuanzisha kituo cha Michezo

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Shule ya Msingi Yongwe kata ya Chanika kuanzisha kituo cha Michezo kwa ajili ya kukuza vipaji vya wanafunzi waweze kupata wachezaji wa vipaji maalum.

Akizungumza katika Bonanza la Shule ya Msingi Yongwe Mwalimu wa Michezo Abdalah Haule ,amesema dhumuni la Bonanza hilo kwa kushirikiana na uongozi wa shule ya Yongwe Chanika mikakati yao kuunda kituo cha Michezo kitakacho kuwa kinawaunda wachezaji wa vipaji wa shule hiyo watakaokuwa wanashiriki mashindano mbali mbali kitaaluma kwa shule za msingi ikiwemo michezo ya umoja wa shule za Msingi (UMITASHUMTA)

“Mikakati yangu nikiwa kama Mwalimu wa michezo tutashirikiana na uongozi wa shule ya Yongwe kuanzisha kituo cha michezo kitakacho kuwa kinawaunda wachezaji wa vipaji wa shule hii waweze kuwa wachezaji bora wa mashindano ya Taifa baadae ambao wataibuka kutokea shule hii “amesema Haule

Abdalah Haule amesema sekta ya michezo ipo katika damu yake ndio alipata msukumo kuanzisha Bonanza hilo la michezo huku akiwa na malengo makuu ya kuunda kituo cha Michezo kitakachowapika vijana wa Yongwe ambapo alisema mikakati hiyo anashirikiana na Chama cha Mapinduzi CCM pamoja na Jumuiya zake ikiwemo Umoja wa Vijana UVCCM Yongwe .

Mkuu wa Yongwe Odilia Chonya, amesema wakiwa wanamichezo wazuri wanafanya vizuri Darasani kitaaluma ambapo aliwataja wasome na kushiriki katika sekta ya Michezo.

Mwalimu Odilia Chonya amewataka kila Jumamosi wanafunzi wote kuja shuleni ndio siku yao maalum ya kufanya michezo shule ili waweze kutafuta vipaji vya wachezaji shuleni.

Amesema michezo ya UMITASHUMTA yatakapoanza mwakani shule hiyo ya Yongwe itakuwa tayari ina timu yake yake ya mpira Wanawake Yongwe Qeen na mpira miguu wanaume ikiwemo na michezo mbalimbali.

Kaimu Katibu wa UVCCM Yongwe Mwinyi Salum amepongeza waandaaji wa Bonanza hilo kwa ajili ya kuandaa vijana katika sekta ya Michezo ambapo alisema vijana wakifanya vizuri wataibuliwa wenye vipaji kutoka chanika .

Kaimu Katibu wa Umoja vijana Mwinyi alisema Umoja wa Vijana Yongwe tumetoa baraka zote katika Bonanza hilo la kukuza vipaji na malengo yao yaweze kufanikiwa .