Na Heri Shaaban,Timesmajiraonline,Msongola
MWENYEKITI wa Serikali ya Mtaa Mvuleni kata ya Msongola wilayani Ilala, Hamis Meja amepokea wanafunzi 350 katika shule mpya ya msingi Mvuleni.
Akizungumza wakati wa kupokea wanafunzi wa shule hiyo mpya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mvuleni,Hamis Meja amesema shule hiyo mpya katika mtaa huo ni matunda ya Serikali ya awamu ya sita ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ambapo amepokea kilio cha mtaa huo kupata shule yao ya msingi ya kwanza toka upatikane Uhuru mwaka 1961.
“Dkt.Samia Suluhu Hassan ametujengea shule mpya ya msingi tulipata eneo hili Serikali imetoa fidia shilingi milioni 150 wakaanza ujenzi rasmi wa kujenga madarasa hii ni kazi kubwa Rais katika utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM,”amesema Hamis.
Mwenyekiti Meja amesema mtaa Mivuleni una watu zaidi ya 12000 mtaa huo ulikuwa hauna shule kwa sasa shule imepatikana Mkuu wa wilaya Edward Mpogolo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Elhuruma Mabelya Afisa Elimu msingi wamefanya kazi kubwa na Jumatatu ya Mei 5,2025 wanafunzi wanaanza rasmi kusoma.
Alimpongeza Mwalimu Mkuu wa shule hiyo kwa usimamizi mzuri ikiwemo kupokea wanafunzi katika kuwaandikisha katika shule hiyo mpya .
Aliwataka Wazazi kuwapa ushirikiano Walimu wa shule hiyo sambamba na kumshukuru Rais Dkt.Samia kwa kazi kubwa aliofanya katika sekta ya eiimu ambapo amejenga shule nyingi za elimu msingi na sekondari.
Alitumia fursa hiyo kumuomba Rais awajengee Shule ya msingi ya Ghorofa kutokana na eneo hilo wakijenga gorofa wataweza kukata eneo la viwanja vya mchezo.
Mwalimu mkuu wa shule Mvuleni Eldhabeth Mtambo alisema shule hiyo inaanza rasmi kufundisha wanafunzi wa darasa la kwanza mei mwaka huu 2025 ambapo imatarajia kuanza kufundisha wanafunzi zaidi ya 350.


More Stories
Mhandisi Manyanya ahoji kifuta machozi walikamatwa na mamba
Waziri Abdallah Ulega awasilisha Bajeti ya Trilioni 2.28Â
Balozi Kaganda ahimiza ushirikiano kwa watumishi wa ubalozi